Home Habari za michezo AHMED ALLY : USAJILI WETU TUTAUTANGAZA MCHANA KWEUPE..SIO KAMA HAO WANAFANYA USIKU...

AHMED ALLY : USAJILI WETU TUTAUTANGAZA MCHANA KWEUPE..SIO KAMA HAO WANAFANYA USIKU USIKU KAMA WANAKULA DAKU…


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally, amethibitisha klabu hiyo inaendelea kufanya usajili wa Wachezaji Kimya Kimya kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kimataifa, inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Simba SC imekua klabu pekee iliyoendelea kuwa kimya katika kipindi hiki cha usajili, huku ikimtambulisha Mchezaji mmoja Moses Phiri anayecheza nafasi ya Ushambuliaji kutoka Zanaco FC ya Zambia.

Ahmed Ally amekua akitoa taarifa za usajili katika kurasa zake za Mitandao ya Kijamii karibu kila siku, huku akiwahimiza Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kuendelea kuwa na Subra.

Katika andiko lake leo Jumatano (Julai 06), Ahmed ameandika: Najua unajiuliza maswali mengi kuhusu usajili wa timu yetu 🦁🦁

Niwatoe hofu wana SIMBA wenzangu tumekamilisha sajili kadhaa za viwango vya CAF

Usajili wetu unaenda kitalaamu sana kwa sababu wachezaji tunaowachukua sio wale waliotemwa na klabu zao

Punde si punde tunaanza kuweka hadharani wachezaji wetu na utambulisho wa wachezaji wetu tutaufanya mchana kweupe sio usiku wa manane kama tunakula daku!!

SEMAJI ASIYEGOMBANA NA WAKUBWA

SOMA NA HII  BUMBULI - HATA TUKIFUNGWA NA SIMBA TUTAENDELEA KUWA NA FURAHA TU...