Home Habari za michezo BAADA YA KASEKE, BALAMA NA YAASSIN KUPIGWA CHINI YANGA….MASTAA WENGINE WALIOKALIA KUTI...

BAADA YA KASEKE, BALAMA NA YAASSIN KUPIGWA CHINI YANGA….MASTAA WENGINE WALIOKALIA KUTI KAVU HAWA HAPA….


Mashabiki wa Yanga bado wanaendelea kushangweka baada ya timu hiyo kubeba mataji matatu, huku wakiendelea kusikilizia mastaa wapya watakaoshuka kikosini kwa msimu ujao, lakini tayari imefahamika beki wa kushoto, Yassin Mustafa anachwa kumpisha Joyce Lomalisa ambaye muda wowote atakuja Jangwani.

Yassin aliyesajiliwa na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea Polisi Tanzania, ni kati ya wachezaji sita ambao watapewa mkono wa kwaheri Jangwani na nafasi yake itachukuliwa na Lomalisa aliyesajiliwa kutoka DR Congo.

Habari za kuamini kuwa ndani ya Yanga, zinasema Yassin ni kati ya wachezaji sita wa kikosi cha sasa watakaotemwa akiwamo Chico Ushindi ambaye awali ilielezwa huenda angebakishwa kwa kazi kubwa aliyoifanya mwishoni mwa msimu na kumfurahisha Kocha Nasreddine Nabi anayetuliza akili kwa sasa katika Mbuga ya Serengeti pamoja na familia yake.

Mbali na nyota hao wengine ambao hawatakuwa kwenye kikosi hicho kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika ni Heritier Makambo, Paul Godfrey ‘Boxer’, Deus Kaseke, Mapinduzi Balama na Yacouba Songne atakayetolewa kwa mkopo kama tulivyodokeza katika gazeti la jana.

“Yassin ni kati ya wachezaji watakaotemwa kwa msimu ujao, akiwamo Chico na Makambo, wengine wameshataarifiwa na wameanza kujiunga na timu nyingine kama ilivyo kwa Boxer,” klilisema chanzo hicho

SOMA NA HII  YANGA YAFUNGUKIA ISHU YA UBINGWA WA SIMBA