Home Habari za michezo BAADA YA KUMALIZANA NA SINGIDA BIG STARS..METACHA MNATA AIBUKA NA KUANIKA HAYA...

BAADA YA KUMALIZANA NA SINGIDA BIG STARS..METACHA MNATA AIBUKA NA KUANIKA HAYA YASIYOFAHAMIKA NA WENGI…


BAADA ya kipa, Metacha Mnata kutambulishwa Singida Big Stars, amesema anachokizingatia ni kazi tu, ndio maana huduma yake inaonekana muhimu kwa timu zinazomtaka.

Hivi karibuni kupitia mtandao wa kijamii (Instagram) ya Singida Big Stars, miongoni mwa wachezaji waliyowatambulisha ni Metacha ambaye amesema mashabiki wasubiri kuona mchango wake.

“Ninapotoka timu moja kwenda nyingine ifahamike ni kazi ndiyo inafanya nionekane sehemu mbalimbali, nashukuru Mungu Polisi Tanzania nimefanya nao kazi vizuri msimu uliyoisha, hivyo maisha mengine yataendelea,” amesema Metacha na kuongeza;

“Ninachokizingatia kwenye karia yangu ni nidhamu, kujituma na kujitambua, naamini hivyo vinanisaidia kulinda kiwango changu.”

Mbali na hilo, amesema msimu uliyoisha umempa taswira ya nini afanye kufanya maandalizi ya msimu ujao, kuhakikisha huduma yake inakuwa muhimu kwenye timu.

“Mapumziko yangu muda mwingi nitautumia na familia yangu na nitakuwa nafanya mazoezi mepesi, baada ya hapo nitasubiri ratiba ya kuingia kambini,” amesema.

SOMA NA HII  DABO AKAZA NA AZAM AFUNGUKA HAYA KUHUSU MECHI DHIDI YA YANGA