Home Habari za michezo BAADA YA KUMTAMBULISHA MBURUNDI WA NEWCASTEL JANA…MASHINE NYINGINE HII HAPA ITATUA YANGA…BANDO...

BAADA YA KUMTAMBULISHA MBURUNDI WA NEWCASTEL JANA…MASHINE NYINGINE HII HAPA ITATUA YANGA…BANDO MUHIMU…


Mapema jana asubuhi, Yanga SC ilimpokea beki wa kushoto raia wa DR Congo, Joyce Lomalisa Mutambala kwa ajili ya kujiunga rasmi na timu hiyo.

Mkongo huyo anajiunga na Yanga akitokea Bravos do Maqui ya Angola. Pia amewahi kucheza GD Interclube ya Angola, AS Vita (DR Congo) na Mouscron (Ubelgiji).

Yanga imelazimika kumshusha beki huyo baada ya kumkosa mbadala mzuri wa kucheza eneo la kushoto.

Lomalisa amepewa mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, huku ikiripotiwa kwamba kwa mwezi anatarajiwa kulipwa shilingi milioni sita.

Kwa muda wa miaka miwili akiwa anaitumikia Yanga, jumla atakuwa amepokea mshahara wa shilingi milioni 144 hadi kumalizika kwa mkataba wake huo.

SOMA NA HII  TWIGA STARS WANA 'MZUKA' KAMA WOTE....WAKAMILIKA KUIMALIZA NAMIBIA KWAO