Home Habari za michezo BAADA YA MASHABIKI KUUPONDA USAJILI WAKE….IVO MAPUNDA AIBUKA NA UJUMBE HUU KWA...

BAADA YA MASHABIKI KUUPONDA USAJILI WAKE….IVO MAPUNDA AIBUKA NA UJUMBE HUU KWA KYOMBO…AMTAJA GEORGE MPOLE…


MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Habibu Kyombo ameshauriwa kupuuzia wanaomdhihaki kwamba kiwango chake si cha kuichezea timu hiyo na kuiga mfano wa beki Joash Onyango aliyedaiwa kuwa ni mzee.

Simba imesajili Kyombo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mbeya Kwanza huku baadhi ya mashabiki wakionekana kuguna. Akizungumza  kipa wa zamani wa Simba na Yanga, Ivo Mapunda alisema, ni wakati wa Kyombo kuwajibu wale wote wanaomsema kwa vitendo ili waamini hajasajiliwa kwa bahati mbaya.

“Mashabiki wa Simba na Yanga ndivyo walivyo hata sisi tulikutana na vitu kama hivyo lakini tulipambana na kuwaaminisha tunaweza, aache kusikiliza maneno yao ya mitandaoni yatamtoa kwenye njia kabisa,” alisema Ivo na kuongeza afanye zaidi ya George Mpole aliyeshangaza wengi msimu huu.

Naye kocha Kenny Mwaisabula alisema, hajapendezwa na kitendo anachofanyiwa mchezaji huyo kisa mzawa jambo ambalo halina afya kwenye soka nchini.

“Huyu Kyombo anahukumiwa na rekodi ya timu alizowahi kucheza huko nyuma zilizoshuka daraja, lakini mashabiki wanatakiwa kujua timu inaweza kushuka ila mchezaji wake akawa vizuri,” alisema Mwaisabula.

Staa wa zamani wa Simba, Mohamed Banka alisema kinachozungumzwa juu yake kimfunze kujipanga kuwafunga midomo kwa vitendo.

“Mchezaji ndiye anayetakiwa kuondoa kejeli juu yake aige mfano wa Onyango wakati anaingia aliitwa babu uwezo wake ukamfanya aitwe nusu mtu, nusu chuma,”

“Kuna dhana ya kutowaamini wachezaji wazawa, lakini awaangalie wenzake akina Bakari Mwamnyeto wamefanya makubwa hivyo asichanganyikiwe, ameingia kinyonge Simba kazi yake imfanye awe shujaa,” alisema Banka.

Msimu huu Kyombo amemaliza ligi akiwa amefunga mabao sita na asisti tatu. Wadau wa soka wanaamini kwamba mchezaji huyo atafanya mambo makubwa na kuwashangaza mashabiki kutokana na Simba mpya ilivyo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WAARABU...DILUNGA AUNGANA NA CHAMA...JOHN BOCCO ATIA WASIWASI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here