Home Habari za michezo DAU LA USAJILI WA OKRAH NDANI YA SIMBA NI ZAIDI...

DAU LA USAJILI WA OKRAH NDANI YA SIMBA NI ZAIDI YA KUFURU…ILIBAKI KIDOGO TU YANGA WANGEPITA NAYE KIBABE…

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ na Mjumbe wa Kamati ya Usajili, Crescentius Magori kwa pamoja walifunga safari hadi Ghana ili kumsajili kiungo mshambuliaji Augustine Okrah na imebainika mchezaji huyo ameikamua Simba mamilioni ya fedha.

Taarifa kutoka ndani
ya Simba ni kwamba Okrah aliyekuwa akikipiga Bechem United ya kwao Ghana, alikuwa na mkataba na klabu hiyo, hivyo kuwafanya mabosi wa Msimbazi kuununua na kulipishwa dola za kimarekani 200,000 ambazo ni zaidi ya Sh 460milioni za Kitanzania.

Okrah alikuwa bado na mkataba wa mwaka mmoja, huku pia akiwa anawindwa na klabu nyingine ya Uarabuni sambamba na Yanga, kitu kilichowafanya mabosi hao wawili wa juu Simba kulipa gharama hiyo pamoja na kumpatia maslahi ambayo mchezaji alikuwa anahitaji ili kukubali kusaini.

Inaelezwa baada ya mvutano wa maslahi pande zote tatu Simba ilikubali kulipa Dola za Kimarekani 200,000 ili kumng’oa Bechem.

Mabosi hao wa Simba walipewa mkwanja huo na muwekezaji wao, Mohammed ‘Mo’ Dewji ili kuhakikisha wanampata Okrah ambaye pamoja na klabu yake walikataa kuchukua pesa chini ya hiyo na mwisho wa siku waliipata saini yake.

Pengine kama si nguvu ya Mo Dewji kutoa kiasi hicho cha pesa, Try Again na Magori wangerudi nchini bila ya kuipata saini Okrah ambaye alionekana kuwa mkali katika masuala la kimaslahi.

Inaelezwa baada ya Mo Dewji kulipa mkwanja huo mrefu Try Again na Magori walirudi nchini na mkataba wa Okrah na siku mbili mbele watani wao Yanga nao walituma ofa ya kumtaka mchezaji huyo aliyeanza kutupia katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ismaly iliyopigwa juzi mjini Ismailia na kuisha kwa sare ya 1-1.

“Tafsiri yake kama tungerudi bila ya kumsainisha Okrah huenda Yanga ingefanikiwa kumpata kwani wao walikuwa na kiasi hicho cha pesa mkononi tayari, bila ya Mo Dewji sijui ingekuwaje,” alisema na kuongeza kigogo huyu mwenye nguvu ya uamuzi ndani ya Simba;

“Okrah kuna mechi ya fainali alicheza kwao hakumaliza baada ya kupewa kadi nyekundu, kuna timu kutoka Sweden iliwafuata viongozi wa Bechem ikiwa tayari kumnunua mchezaji huyo kwa Dola 600,000 zaidi ya Sh1.2 Bilioni.

SOMA NA HII  TWIGA STARS WANA 'MZUKA' KAMA WOTE....WAKAMILIKA KUIMALIZA NAMIBIA KWAO

Viongozi wa Bechem waliifahamisha hiyo timu kwamba Okrah tayari ameshauzwa kwetu. Na jamaa sababu walikuwa siriazi wanamtaka, walituma maombi yao kwetu na ofa hiyo ya Sh1.2 bilioni, lakini tulikataa kutokana na malengo yetu ya msimu ujao,” alisema na kuongeza;

“Tulikataa pesa hiyo ndefu sababu msimu uliopita hatukufanya vizuri kwahiyo tunahitaji mchezaji kama Okrah mwenye uwezo ili kutufikisha kwenye malengo yetu ya kufanya vizuri msimu ujao.”

Akizungumza kabla ya kwenda kambini Misri, Okrah alisema kwanza amefurahi kujiunga na timu kubwa Afrika kama Simba kwani ilikuwa moja ya ndoto zake na anaamini anaweza kufanya vizuri zaidi na akapata ofa nyingine kubwa zaidi ya wakati huu.

“Baada ya kumalizana na Simba sikutaka tena kusikia lingine lolote, ni kweli kuna timu mbili za Ulaya zilikuja ila naamini nikionyesha ubora hapa Simba nitapa nyingine zaidi ya hizo,” alisema Okrah na kuongeza;

“Nipo Simba kuhakikisha nafanya vizuri zaidi ya nilipotokea ili msimu ujao timu ifikie malengo yake.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here