Home Habari za michezo DODOMA JIJI HAWAPOI WALA HAWABOI….WAENDELEA KUSHUSHA MAJEMBE YA NGUVU…SIMBA NA YANGA ZIJIANGALIE…

DODOMA JIJI HAWAPOI WALA HAWABOI….WAENDELEA KUSHUSHA MAJEMBE YA NGUVU…SIMBA NA YANGA ZIJIANGALIE…


DODOMA Jiji bado haijamaliza usajili!  Hii ni baada ya kumnasa winga mshambuliaji, Salum Kihimbwa kutoka kwa “wakata miwa” Mtibwa Sugar.

Usajili wa Kihimbwa unathibitisha kuondoka kwa kiungo Mcha Khamis ‘Vialli’ na ndio uliochukua muda mrefu zaidi kutimia kwa timu hiyo iliyomuwinda muda mrefu hadi kufikia makubaliano ya kumvuta kukipiga jijiji Dodoma.

Ili kumng’oa Mtibwa, usajili wa Kihimbwa ni miongoni mwa ulioigharimu kiasi kikubwa zaidi Dodoma Jiji kwenye dirisha hili la usajili unaoendelea, kuanzia dau la kumsajili na mshahara watakaomlipa winga huyo machachari.

Kihimbwa anaungana na nyota wapya Daniel Mgore, Jimmy Shoji, Amaan Kyata, Christian Zigah, Collins Opare, Hassan Mwaterema, Paul Peter.

Wengine ni Rashid Chambo, Randy Bangala na Mwana Kibuta huku ikibaki wachezaji wasiozidi watatu kufunga usajili.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo mbioni kutambulishwa wakati wowote ni beki Hassan Kessy pamoja na kipa mmoja mpya atakayechukua nafasi ya Mohammed Yusuph na Hussein Masalanga waliotemwa.

Hassan Kessy aliyemalizana na KMC, ‘amejiunga’ na timu hiyo kama beki wa kulia kuchukua nafasi ya George Wawa aliyeondoka ndani ya timu hiyo.

SOMA NA HII  UONGOZI WA SIMBA WAFUNGUKA MAZITO KUHUSU PHIRI KUTOKUCHEZA