Home Habari za michezo HIVI NDIVYO SAKHO NA TUZO YAKE WALIVYOPOKELEWA MISRI NA MASTAA WA SIMBA…AMKIMBILIA...

HIVI NDIVYO SAKHO NA TUZO YAKE WALIVYOPOKELEWA MISRI NA MASTAA WA SIMBA…AMKIMBILIA KAPOMBE NA KUMKUMBATIA…


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Ousmane Sakho amewasili nchini Misri kujiunga na wenzake katika kambi ya maandalizi wakijiandaa na msimu mpya 2022/2023.

Sakho amewasili nchini Misri akiwa na tuzo yake ya Goli Bora la mwaka la CAF 2022, alipoibuka kidedea usiku wa Julai 21, mjini Rabbat nchini Morocco.

Alipofika Kambini Sakho alimtafuta Mlinzi Shomari Kapombe na kushangilia nae kwa nguvu huku ikifahamika pasi ya goli hilo ilitoka kwa Kapombe.

Sakho alifunga goli lililobeba tuzo dhidi ya ASEC MIMOSAS katika mchezo wa hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho, katika Dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

SOMA NA HII  WAKATI ZAIDI YA MAKOCHA 80 WAKIOMBA KAZI...KOCHA MPYA SIMBA NI HUYU HAPA...UONGOZI WATOA TAMKO RASMI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here