Home Habari za michezo KISA RONALDO…MESSI AWAPIGWA MKWARA PSG…AWAAMBIA WAKIMSAJILI TU..NA YEYE ANASEPA SIKU HIYO HIYO…

KISA RONALDO…MESSI AWAPIGWA MKWARA PSG…AWAAMBIA WAKIMSAJILI TU..NA YEYE ANASEPA SIKU HIYO HIYO…


Ripoti zinaeleza kuwa, staa wa Paris Saint-Germain, Lionel Messi, ametishia kuondoka kikosini hapo endapo klabu hiyo itamsajili Cristiano Ronaldo.

Kwa sasa Ronaldo anatajwa kuondoka Manchester United, huku PSG ikiwa ni kati ya timu ambazo zinatajwa kumuwania sambamba na Chelsea na Bayern Munich.

Imeelezwa kuwa, hakuna uhakika kama PSG itatishika na suala hilo la Messi kwani timu hiyo inataka kujipanga kuona inafanya kweli katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini imeelezwa kuwa, uwepo wa Kylian Mbappe kwenye projekti mpya kunaweza kumvuta Ronaldo ndani ya kikosi hicho, Messi na Ronaldo wamekuwa washindani wakubwa kwenye soka ambapo wanatajwa kuwa ni wachezaji wenye rekodi za kutisha.

Ronaldo anashika nafasi ya pili kwa wachezaji wenye Ballon D’or nyingi akiwa nazo tano, huku Messi akiongoza akibeba saba.

SOMA NA HII  IHEFU NA SIKU 60 ZA MACHUNGU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here