Home Habari za michezo KISA UBINGWA WA YANGA…KANDORO AIBUKA NA KUANIKA NJIA ZOTE ZA SIRI ZILIZOTUMIKA…AFUNGUKA...

KISA UBINGWA WA YANGA…KANDORO AIBUKA NA KUANIKA NJIA ZOTE ZA SIRI ZILIZOTUMIKA…AFUNGUKA A-Z KILICHOTOKEA…


MTEGO wa viwanja vigumu walioutegua Yanga msimu huu 2021/22 ndio uliowapa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya 28 na kuendeleza ubabe kwa watani zao Simba waliochukua mara 22.

 Yanga imetwaa ubingwa wa ligi hiyo bila ya kupoteza mchezo hata mmoja ambao waliukosa mara nne mfululizo ukienda kwa watani wao.

Mkurugenzi wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Thabit Kandoro alisema kuwa, kabla msimu haujaanza walikaa na kupanga mipango mikakati ya namna gani timu yao itwae ubingwa huo.

Alisema katika mipango hiyo walibaini njia ya kutoboa ni kukabiliana na ukame kwenye viwanja vinne ambavyo ni Sokoine, Mkwakwani, Karume na Ilulu kwani timu wanazokutana nazo huko daima matokeo huwa magumu.

“Tuliamua kuweka mkakati maalum kwa viwanja hivyo ambavyo timu zake Tanzania Prisons, Mbeya Kwanza na Mbeya City na Namungo huwa zinatupa shida na tulifanikiwa kupenya,” alisema Kandoro.

Kandoro alisema, timu hizo ziliwapa ugumu na ushindani mkubwa wawapo hata nyumbani hivyo kitendo cha kubaini na kuitatua changamoto hiyo ndicho kilichowapa ubingwa.

“Msimu unaokuja utakuwa mgumu sana na wenye ushindani zaidi, tutaendelea kuweka mkazo zaidi ili tutimize lengo letu, lakini sisi tunacheza mechi zetu hatuangalii nani anafanya nini na hicho kimetusaidia pia,” alisema.

Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano sasa Makamu wa Rais Arafat Haji alisema, walipambana kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa kuanzia wachezaji, benchi la ufundi hadi wao viongozi.

“Kila mmoja alitimiza wajibu wake kwa wakati sahihi, tutaendelea hivyo ili kuendeleza tulipoishia msimu huu,” alisema Arafat.

Msimu ulioisha Yanga imechukua makombe matatu, ikianza na Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), makombe ambayo yote yalikuwa yakishikiliwa na Simba.

SOMA NA HII  KWA MKAPA KUMEDODA...MECHI SIMBA NA YANGA MASHABIKI HAKUNA...ISHU NZIMA IKO HIVI