Home Geita Gold FC KUELEKEA MSIMU UJAO….MINZIRO APAZA SAUTI KWA UONGOZI WA GEITA…AFUNGUKA YOTE KUHUSU USAJILI...

KUELEKEA MSIMU UJAO….MINZIRO APAZA SAUTI KWA UONGOZI WA GEITA…AFUNGUKA YOTE KUHUSU USAJILI WA MASTAA WAPYA….


ILI kukabiliana na ushindani katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya Kombe la FA, Geita Gold FC inatarajia kusajili wachezaji wapya nane, imefahamika.

Kocha Mkuu wa Geita Gold FC, Fred Minziro alisema anaamini akipata nyota hao katika nafasi mbalimbali atakuwa na kikosi imara kitakachompa matokeo chanya.

Minziro alisema anaamini ujio mpya wa nyota hao utaimarisha na kikosi chake huku pia akianza maandalizi ya kusaka mechi mbalimbali za kirafiki.

“Ninatarajia kuongeza wachezaji nane kwa ajili ya msimu ujao, ninaendelea kufanya mazungumzo na wachezaji ambao ninawahitaji wajiunge katika timu yetu ili kuunda kikosi chenye ushindani kuelekea msimu ujao,” alisema Minziro.

Kocha hiyo alisema pia mara baada ya kumaliza mchakato wa usajili, atakiweka hadharani kikosi chake na programu rasmi ya mazoezi itakavyokuwa.

“Wiki ijayo tunatarajia kuanza kambi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu itakayoanza Agosti 17, mwaka huu, tutajipanga zaidi ili kupata timu imara,” Minziro alisema.

Aliongeza anafahamu msimu ujao utakuwa na ushindani hivyo amepanga kuingia kambini mapema kwa lengo la kufanya marekebisho ya makosa aliyoyabaini wakati wanamaliza ligi ili kuanza msimu mpya kwa kasi.

Geita Gold FC ilimaliza msimu uliopita ikiwa katika nafasi ya nne na imekata tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  YANGA VS RIVERS UNITED KUKIWASHA LEO...HUJUMA ZAWASHTUA WANANCHI