Home Habari za michezo KUHUSU MAJEMBE MAPYA YANGA…SURE BOY ATIKISA KICHWA ..KISHA AKAFUNGUKA HAYA…AIKUMBUKA AZAM FC...

KUHUSU MAJEMBE MAPYA YANGA…SURE BOY ATIKISA KICHWA ..KISHA AKAFUNGUKA HAYA…AIKUMBUKA AZAM FC …


KIUNGO nyota wa Yanga, Aboubakar Salum Jr ‘Sure Boy’ amesema kwa aina ya mastaa waliotua Yanga mpaka sasa msimu ujao utakuwa balaa.

Staa huyo wa Taifa Stars, amekiri kwamba atahitaji kufanya kazi ya ziada kutetea namba yake lakini anaamini timu hiyo itafanya vizuri zaidi kwenye mashindano yote kuliko misimu iliyopita wakianza na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, Agosti 13.

“Sina hofu yoyote kwa ujio wa mastaa hao zaidi unanipa morali ya kupambana zaidi, uwezo nilionao ukichanganya na uzoefu wa Ligi sina sababu ya kuhofia usajili unaoendelea, nina imani na kipaji changu,” alisema na kuongeza;

“Naheshimu sajili zote, naamini utakuwa chachu ya kufanya vyema na bora kwetu. Kuhusu kucheza, kila mmoja ana umuhimu wake kwa nafasi yake. Nina uhakika wa kucheza najiamini nina kipaji, nimetoka Azam FC vikosi vingi vilipangwa wakiniondoa lakini nimetua nimecheza,” alisema.

Sure Boy alisema anatarajia timu bora na ya ushindani pia msimu ujao wataendeleza walipoishia na watakuwa na matokeo mazuri ndani na nje kutokana na nafasi waliyoipata kushiriki mashindano ya Afrika.

Usajili wa kiungo Gael Bigirimana unazidi kuongeza chachu safu ya kiungo ndani ya Yanga msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kiungo huyo wa Burundi mwenye sifa ya kucheza kama mkabaji na mshambuliaji hata mshambuliaji wa pili kwa namna moja ama nyingine anaweza kuwapa hofu wachezaji wa kikosi cha kwanza Yanga.

Mpaka sasa Yanga ina viungo kama Sure Boy, Feisal Salum, Yanick Bangala, Khalid Aucho na Zawadi Mauya hivyo kama Bigirimana akiwa kwenye fomu basi atapenya katikati yao.

Yanga tayari imewatangaza Bernard Morrison, Gael Bigirimana na Lazarous Kambole na wamethibitisha kusajili wachezaji watano tu katika dirisha hili la usajili.

Wadau wa soka nchini umepongeza usajili wa mchezaji huyo kutokana na rekodi aliyonayo ya kupita katika timu kubwa huku wakiweka wazi ushindani utaongezeka katika nafasi ya kiungo.

Mshambuliaji wa zamani Yanga, Herry Morris alisema ufanisi wake ndio utakaombeba na kumfanya acheze kwenye kikosi cha kwanza lakini anaamini kabisa ushindani utakuwa mkubwa.

SOMA NA HII  MTONYO WA LEO UKO KWENYE UHAKIKA WA ODDS ZA MECHI HIZI....

“Ni usajili ambao utaongeza chachu kwenye eneo la kiungo, kila mmoja anayecheza eneo hilo lazima azidi kupambana kwa sababu wanajua wote waliopo ni wazuri na atakayefanya vyema atapata nafasi ya kucheza,” alisema Morris ambaye ni mchezaji wa zamani wa Prisons ya Mbeya.

Mchezaji wa zamani Simba na Yanga, Zamoyoni Mogella alisema kwa uzoefu, Bigirimana huyo yupo vizuri na bado ana deni la kuonyesha uwanjani kwa sababu mashabiki wa Yanga watakuwa na matumaini makubwa baada ya mchezaji huyo kutambulishwa katika mkutano wao.

“Kuja kwake ushindani unaongezeka kwenye timu na hiyo sio mbaya maana inasaidia timu kufanya vizuri, kikubwa ni yeye kupambana,” alisema Mogella.