Home Habari za michezo MANULA : SIMBA WAMEKUBALI NIONDOKE….HAWANA SHIDA NA MIMI…NINATAMANI NIPATE TIMU…

MANULA : SIMBA WAMEKUBALI NIONDOKE….HAWANA SHIDA NA MIMI…NINATAMANI NIPATE TIMU…


Kipa wa Klabu ya Soka ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania, Aishi Manula amekanusha tetesi za kuongeza mkataba kwenye timu hiyo ambazo zimekuwa zikienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.

Pia, ameeleza kwamba anatamani kupata timu nyingine ambayo ataichezea na yuko huru kuichezea timu yoyote kwani hata uongozi wa klabu ya Simba ambayo anaichezea kwa sasa umesharidhia kuondoka kwake klabuni hapo na endapo kama atapata timu sahihi ya kuichezea basi klabu yake iko tayari kumruhusu bila pingamizi lolote.

“Sidhani kama Simba wamesema nimeongeza mkataba ama mimi nimesema nimeongeza mkataba, kupost picha, mtu anaweza kupost mahali popote. Ile picha alipost meneja wangu, Jemadari Said tukiwa kwenye mazungumzo na sidhani kama alipost akaandika ‘deal done’, maneno ya wachambuzi wawaachie wachambuzi.

“Ninatamani nipate timu na hata Watanzania wanatamani, pia viongozi wa Timu yangu ya Simba wamekuwa wakisema kama ninapata sehemu nzuri wao wapo tayari kuniachia niende, hawana shida na mimi. Viongozi wangu wamekuwa weredi na wenye mawazo chanya wanapenda nipate mafanikio zaidi nje ya Simba,” 

SOMA NA HII  BAADA YA KUKAA MUDA MREFU KIDOGO MOROCCO...KISINDA KAMA CHAMA...AFUNGUKA ISHU YA KURUDI YANGA...