Home Azam FC MSEMAJI WA AZAM FC “ZAKAZAKAZI” AZINANGA TUZO ZA TFF…ADAI BANGALA, NABI, INONGA...

MSEMAJI WA AZAM FC “ZAKAZAKAZI” AZINANGA TUZO ZA TFF…ADAI BANGALA, NABI, INONGA HAWAKUSTAHILI KUSHINDA..


Baada ya Usiku wa jana katika hoteli ya Johari Rotana kutolewa kwa tuzo za TFF 2021/2022 na nyota mbali mbali kujinyakulia tuzo zao.

Sasa leo Julai 8, Afisa Habari wa Klabu ya Azam FC, Thabit Zakaria “Zakazakazi” amekuja na hoja na kuanika kuwa licha ya baadhi ya nyota kama Inonga (beki bora), Bangala (Kiungo bora, mchezaji bora wa msimu) na wengine walioshinda hawakustahili kupewa tuzo hizo.

Zakazakazi anaamini licha ya ubora waliionesha nyota hao bado upande wa pili kulikuwa na sababu za msingi kutopata zawadi wa;izopata siku ya jana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram wa Instagram, Zaka ameandika;

HONGERENI WASHINDI LAKINI…

Tuzo za wanamichezo hutokana na takwimu (Statistics) na haiba + wajihi (Personality)

Washindi wa tuzo wanapaswa kuimbwa kama mashujaa ili wawe mfano kwa kizazi kijacho. Washindi wa tuzo wanatakiwa kuwa poster boys ili kuvutia biashara ya mpira.

LAKINI

Henoc Inonga Bakka ni beki mzuri sana, lakini hakustahili tuzo. Takwimu zinaweza kumbeba lakini haiba na wajihi vinamkataa.

Alimpiga kichwa winga wa Coastal Union, akapata kadi nyekundu. Hiyo ilipaswa kuwa kigezo cha kumtoa kwenye kinyang’anyiro

Shabban Djuma naye ni bonge la beki, lakini hata hivyo hakustahili.Takwimu zake ni bora sana, lakini haiba na wajihi vinamkataa

Alimkanyaga kwa makusudi Yahya Mbegu wa Polisi Tanzania na akafungiwa mechi 3. Hiyo ilitosha kumtoa kwenye mchakato.

Yannick Bangala ni mchezaji aliyekamilika, haina shaka. Takwimu za kuandika na kuona zote ziko upande wake.

Lakini haiba na wajihi vinamkataa. Alionesha ishara ya matusi ambayo haifai kwenye jamii.

Nasridine Nabi, bonge moja la kocha na timu yake imefanya vizuri sana kimbinu msimu huu…ambayo ni kazi yake

Takwimu zote zinaweza kuwa upande wake, lakini haiba na wajihi vinamkataa.

Alifungiwa mechi tatu, kwa mambo yasiyofaa.

Ahmed Arajiga ameshinda tuzo ya mwamuzi bora.Msimu huu mwamuzi huyu alifungiwa kwa kushindwa kuumudu mchezo.

Kwa matendo yao haya, tunataka kizazi kijacho kiwaone hawa ni mashujaa?

SOMA NA HII  ALICHOSEMA BOSI WA GEITA GOLD BAADA YA KUPIGWA 5-0 NA SIMBA...ATANGAZA MSAKO NCHI NZIMA...

Tunataka hawa ndiyo wavutie biashara ya mpira? Tusijali upande wa takwimu pekee na kupuuza upande wa personality kwenye branding.

Turekebishe hilo ili kuzifanya tuzo hizi ziwe bora pasi na shaka.

Mshindi wa tuzo awe kioo cha jamii kweli kweli.

Hongereni washindi wa tuzo. Hongereni kamati, tunaendelea kujifunza!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here