Home Habari za michezo SAA CHACHE BAADA YA KUFUNGIWA NA TFF…MANARA AVUNJA UKIMYA…AIBUKA NA KUANIKA HILI…ADAI...

SAA CHACHE BAADA YA KUFUNGIWA NA TFF…MANARA AVUNJA UKIMYA…AIBUKA NA KUANIKA HILI…ADAI IWE KHERI AU SHARI…..


Saa chache baada ya kuungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi, Msemaji wa Yanga, Haji Manara ametoa kauli yake ya kushukuru.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameposti picha yake akiwa na kombe la kombe la FA walilolitwaa mwaka huu na kusindikiza na ujumbe uliosomeka hivi:

“Iwe ni Jambo la Kheri au Shari, neno langu kuu ni kumshukuru Muumba Mbingu na Ardhi Kwa neno moja kubwa na lenye maana pana sana. AL-HAMDULILLAH ???????? Thanks football.”

Mapema hii leo, Kamati ya Maadili ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imetoa maamuzi kuhusiana na sekretarieti kufungua kesi katika kamati hiyo dhidi ya afisa habari wa Yanga Haji Manara.

Kamati ya maadili ya TFF imemkuta na hatia Haji Manara na kumfungia miaka miwili kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi na faini ya Tsh milioni 20 kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF Wallace Karia.

Haji Manara alipishana kauli ya Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia katika eneo la VVIP wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.

SOMA NA HII  UONGOZI SIMBA WATOA UFAFANUZI HUU JINSI WATAKAVYOPITA NA UPEPO LIGI YA MABINGWA