Home Habari za michezo SAKATA LA KUFUNGIWA NA TFF….AFANDE SELE AMVAA MANARA…ADAI ANATABIA ZA KIPOPO…”TUMTETEE APIGE...

SAKATA LA KUFUNGIWA NA TFF….AFANDE SELE AMVAA MANARA…ADAI ANATABIA ZA KIPOPO…”TUMTETEE APIGE HELA ZAKE”…


Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ amesema kama Watanzania wakiacha ujinga na kufikiri vizuri watagundua, Haji Manara ni popo wa mpira.

Afande amesema Haji alikosea ndio maana alikwenda kuomba msamaha kwa Rais wa TFF Wallece Karia, lakini hata hivyo hukumu aliyopewa ya kifungo cha miaka miwili na faini ya milioni 20 ni kubwa sana na ina mlengo wa kukomoana.

Alisema, watu wa Simba wanatakiwa watambue kwamba hawawezi kufurahia hukumu ya Haji kwa kwa kuamini sio mwenzao wakati wanakumbuka ni Haji huyohuyo alikuwa akiwatukana Yanga SC alipokuwa msemaji wa Simba SC.

Amesema hata watu wa Yanga, hawawezi kusema Haji ni mwenzao wakati wana kumbukumbu ya matusi waliyokuwa wanatukanywa na Haji wakati akiwa Simba.

“Tukubaliane mwenzetu ni popo wa soka, haelewiki ni Simba au Yanga kwa sababu kikawaida mtu huwezi kuhama timu ukiwa na umri wa zaidi wa miaka 40, tunamtetea tu apie hela zake,” alisema Aafande Sele.

SOMA NA HII  YANGA WATUMA UJUMBE KMC, YAWAKUMBUSHA KWAMBA WANAONGOZA LIGI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here