Home Habari za michezo WAKATI SIMBA WAKIPAMBANA NA MANZOKI…MAMELOD SUNDOWNS WASAJILI KIFAA CHA TIMU YA TAIFA...

WAKATI SIMBA WAKIPAMBANA NA MANZOKI…MAMELOD SUNDOWNS WASAJILI KIFAA CHA TIMU YA TAIFA CHILE….


Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imefanikiwa kunasa saini ya kiungo mshambuliaji raia wa Chile, Marcelo Allende.

Kabla ya kutua Mamelodi, Marcelo (23) alitokea klabu ya Montevideo City Torque inayoshiriki ligi Kuu ya Uruguay.

Nyota huyo alikuwa nahodha kwenye timu ya taifa ya Chile (U-17) kwenye mashidano ya Kombe la Dunia kwa vijana 2015.

Katika misimu miwili aliyocheza kwenye klabu ya Montevideo kuanzia 2020 hadi 2022 alicheza jumla ya michezo 87 akifunga mabao 16 na kusaidia (Assisti) 23.

Klabu yake tayari imeshamuaga kiungo huyo mshambuliaji na imemtakia kila la kheri kwenye safari yake ya soka.

SOMA NA HII  ZA NDANIII KABISAAA...NTIBAZONKIZA, KASEKE KUKIPIGA NA DTB FC MSIMU UJAO...STAA MWINGINE JINA KUBWA HUYU HAPA......

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here