Home Habari za michezo WAKATI WENZAKE SIMBA WAKIWA NA MAWAZO TOFAUTI….MANULA ANYOOSHA MIKONO JUU KWA YANGA…ATAJA...

WAKATI WENZAKE SIMBA WAKIWA NA MAWAZO TOFAUTI….MANULA ANYOOSHA MIKONO JUU KWA YANGA…ATAJA WALIPOFELI…


Kipa wa Klabu ya Soka ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania, Aishi Manula amekiri kuwa watani wao wa Jadi, Yanga sc waliwazidi sehemu kubwa katika msimu uliomaliza jambo lililowafanya kunyakuwa mataji matatu ya msimu.

Manula amesema hayo wakati akihojiwa kwenye usiku wa tuzo za mastaa wa soka zilizofanyika usiku wa jana jijini Dar es Salaam.

“Msimu ulikuwa mzuri na wa ushindani, lakini kwa bahati mbaya malengo tuliyojiwekea kama Klabu hayakutimia, kwa hiyo tunaweza kusema ulikuwa msimu mbaya kwetu.

“Kama klabu na wachezaji tuliweka nguvu kubwa kwenye mashindano ya kimataifa ili kupiga hatua zaidi kutofautisha na misimu iliyopita, lakini kwa bahati mbaya hatukuweza kufanikiwa kile tulichokipanga. Yote kwa yote kuna tunamshuru Mungu.

“Yanga walituzidi kiujumla kama timu, ukiangalia sisi kwa takribani miaka mitano tumekuwa tukicheza back to back mashindano ya Kimataifa kasoro ule msimu mmoja ambao tulitoka mapema lakini misimu mingine tulifanya vizuri na tukafika robo fainali.

“Wenzetu hawakuwa na mashindano ya kimataifa hivyo sisi tulikuwa tukitoka Kimataifa tunaunganisha kwenye ligi, hata ukipata majeruhi hapati muda wa ku-recover lakini wao walikuwa na muda wa kutosha kupumzika na kurejea wakiwa na nguvu zaidi,” amesema Manula.

SOMA NA HII  YANGA WATUMIA MTETEMO WA MEYELE KUWATISHA SIMBA...BUMBULI AZIDI KUTAMBA 'KIBABE'....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here