Home Habari za michezo ACHANA NA SABABU ZA VIJIWENI..HUU HAPA UKWELI WA SIMBA NA YANGA KUANZIA...

ACHANA NA SABABU ZA VIJIWENI..HUU HAPA UKWELI WA SIMBA NA YANGA KUANZIA HATUA YA AWALI KLABU BINGWA AFRIKA…


Juzi Jumanne usiku, ilifanyika droo ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika na lile la Shirikisho huku wawakilishi wa Tanzania Simba, Yanga, Azam na Geita Gold wakitambua wapinzani wao.

Yanga, Simba wanaiwakilisha nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Azam na Geita Gold zinashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Swali kubwa kwa wadau wengi nchini limekuwa ni kwanini Simba anaanzia hatua za awali (Preliminary) licha ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo msimu uliopita ambapo waliishia hatua ya robo fainali.

Baada ya hilo Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetoa mwongozo wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) na kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) kwa msimu ujao wa 2022/2023.

Kutokana na mwongozo huo, Simba na Yanga zitaanzia raundi ya awali (Preliminary) huku Azam FC wao wataanzia raundi ya kwanza na Geita Gold FC itaanzia raundi ya awali kwenye Kombe la Shirikisho.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ni timu sita (6) tu ambazo ni Al Ahly (Misri), Raja Club Athletic, Wydad Athletic Club (Morocco), TP Mazembe (DR Congo), Espérance Sportive de Tunis (Tunisia) na Mamelodi Sundowns FC (Afrika Kusini) kati ya zile 58 ambazo zitaanzia raundi ya kwanza na timu zingine zitaanzia raundi ya awali.

Kombe la Shirikisho ni timu 13 tu RS Berkane (Morocco), USM Alger, JS Saoura (Algeria), G.D. Sagrada Esperança (Angola), Pyramid (Misri), Motema Pembe (DR Congo), Accra (Ghana), Marumo Gallants F.C. (Afrika Kusini), CS Sfaxien, Club Africain (Tunisia), CS Constantine (Algeria), Azam FC (Tanzania) na Zesco FC ya Zambia zitakazoanzia raundi ya kwanza kati ya timu 51.

Msimu huu 2022/2023, Ligi ya Mabingwa Afrika zitashiriki timu 58 huku zikitakiwa timu 32 kushiriki raundi ya kwanza na zile 32 zingine unapata jumla ya 64 ambazo ukitoa idadi ya zinazoshiriki unapata sita tu ambazo zitaanzia hatua ya kwanza. Simba haitaanzia raundi ya kwanza kwa sababu ipo nafasi ya 10 kati ya timu 58 zinavyoshiriki ligi hiyo.

SOMA NA HII  JOHN BOCCO AWEKA KANDO TUZO YA UFUNGAJI BORA

Msimu uliopita ligi ya Mabingwa Afrika ilishirikisha timu 54 na Simba ilikuwa nafasi ya 10 kati ya zilizoshiriki ambazo timu 64 ukitoa 54 unapata idadi hiyo ndio maana zilianzia raundi ya kwanza kwa msimu huo ulioisha.

Timu 52 kati ya 58 zitaanzia raundi ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika na 26 zitafuzu raundi ya kwanza na kuungana na zile sita ambazo zinaanzia raundi ya kwanza na kuwa jumla ya 32 (26+6=32) hii ni kutokana na CAF msimu huu limeongeza klabu nne kushiriki ligi hiyo tofauti na msimu uliopita.

Azam inaanzia raundi ya kwanza kutokana na kuwa miongoni mwa klabu 13 bora kati ya 51 zinavyoshiriki Kombe la Shirikisho msimu huu, maana yake ni kwamba raundi ya kwanza zinatakiwa 32 ambapo ukizidisha mara mbili unapata 64.

Kama haitoshi ukichukua idadi hiyo na kuitoa kwa 51 unapata 13 ndio maana klabu 13 zinazoshirikiki michuano hiyo zinaanzia raundi ya kwanza.

Hivyo klabu 38 zitaanzia raundi ya awali kwenye Kombe la Shirikisho na 19 zitafuzu raundi kwanza na kuungana na timu 13 na kuwa timu 32 (19+13=32).

Akizungumza juu ya mabadiliko hayo, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alisema wanaheshimu kanuni na utaratibu uliopangwa na CAF, hivyo watapambana ili kufanya vizuri bila kujali wanaanzia hatua gani