Home Habari za michezo BAADA YA KUFUNGA GOLI JUZI…MORRISO ‘AANZA KUKERA’ YANGA…ATUPA JIWE LA GIZANI KWA...

BAADA YA KUFUNGA GOLI JUZI…MORRISO ‘AANZA KUKERA’ YANGA…ATUPA JIWE LA GIZANI KWA AZAM FC…


Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga ambaye ni raia wa Ghana, Bernard Morrison amesema wanafahamu kuwa mechi yao ijayo dhidi ya Azam FC itakuwa ngumu lakini kutokana na ubora wa kikosi chao na maandalizi waliofanya, watahakikisha wanapambana ili kupata matokeo.

Mechi hiyo ya mzunguko wa tatu wa Ligi Kuu ya NBC imepangwa kupigwa katika Dimba la Mkapa, mnamo Septemba 6, 2022 ambapo Yanga atakuwa mwenyeji. Mpaka sasa Yanga ana pointi 6 akiwa ameshinda mechi zake mbili za awali alizocheza ugenini huku Azam akiwa na pointi 4 baada ya kushinda mechi moja na kutoa sare mechi moja.

“Kila mmoja wetu anajitahidi kujiandaa kuwa tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Azam FC, ndio maana tupo hapa. Tulidhani kwamba tunakwenda kupata mapumziko mafupi lakini kutokana na ukubwa wa mechi hiyo tunalazimika kusalia kambini na kufanya mazoezi kujiandaa na mechi hiyo.

“Mechi dhidi ya Azam ni kubwa lakini kama unavyojua Yanga ni timu kubwa yenye ubora na wachezaji wazuri ambao sote tupo tayari kwa lolote. Hakuna shida yoyote kwenye kikosi kwa sababu kila mmoja wetu anafahamu umhimu wa mechi hii,” amesema Morrion.

Akizungumzia kuhusu mchezo wao wa michuanoi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya kwanza ya mtoano dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini, Morrison amesema;

“Yanga tayari ni mabingwa wa Taifa, kwa hiyo lengo letu sasa ni kufanya vizuri katika mashindani ya kimataifa. Mechi hiyo ni muhimu kwa kila mmoja wetu kwenye timu na sote tunajua umhimu wake. Tutakwenda kupambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri ndani ya uwanja.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA KUTEMANA NA YANGA...NTIBAZONKIZA APANGA KUTAPIKA NYONGO..."SITARUHUSU MTU ANICHAFUE"...