Home Habari za michezo BAADA YA KUIFUNGISHA MDOMO YANGA…MASTAA VIPERS WAIBUKA NA KUWAPONDA KINA AZIZ KI…

BAADA YA KUIFUNGISHA MDOMO YANGA…MASTAA VIPERS WAIBUKA NA KUWAPONDA KINA AZIZ KI…


Wachezaji wa Timu ya Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda, Vipers Sc wameaponda mabeki wa Yanga wakisema kuwa hawana kasi ndio maana ilikuwa rahisi kwao kupenya kirahisi ngome ya Yanga na kuwatungua kirahisi.

Wachezaji hao wamesema hayo wakihojiwa na wanahabari mara baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Vipers na Yanga kukamilika katika Dimba la Mkapa na Vipers kuibuka na ushindi wa bao 2-0 juzi Jumamosi, Agosti 6, 2022.

“Yanga watengeneze timu kwanza, hata sisi tulikuwa hivyo hivyo lakini tukatengeneza timu yetu polepole mpaka hapa ilipofikia leo.

“Tatizo tuliloiona kwa Yanga ni mabeki wao hawana kasi, sisi washambuliaji wetu wana kasi ndio maana walikuwa wanawaacha mabeki wa Yanga. Sisi mechi ya leo (juzi) imetuongezea nguvu na maandalizi yetu yalikuwa mazuri,” wamesema wachezaji hao.

Kwa upande wake straika aliyekuwa akihusishwa kutua Simba, Cesar Manzoki amesema; “Japo sijacheza lakini tumeshinda bao 2-0, mechi ilikuwa nzuri sana, tunaiheshimu Yanga ni timu nzuri.”

Mabao ya Vipers yalifungwa na Milton Karisa dakika ya kwanza ya mchezo huku bao la pili likifungwa na Anukani Bright dakika ya 64.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA SIMBA KUIZABUA HOROYA 7-0...TRY AGAIN AFUNGUKA MAGUMU WALIYOPITIA...