NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mechi za ugenini zilikuwa ni ngumu ila wanachofurahia ni kupata matokeo chanya.
Mechi ya kwanza kwa msimu wa 2022/23 ilikuwa dhidi ya Polisi Tanzania ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ulisoma Polisi Tanzania 1-2 Yanga na ule wa pili ulisoma Coastal Union 0-2 Yanga.
Kinara wa utupiaji ndani ya Yanga ni Fiston Mayele ambaye ana mabao mawili huku Bernard Morrison na Bakari Mwamnyeto wakiwa wametupia bao mojamoja.
Nabi amesema:”Haikuwa kazi rahisi kupata matokeo kwenye mechi zetu mbili hasa ukizingatia kwamba wachezaji walikuwa na uchovu na kila timu ambayo tunapambana nayo ilikuwa inahitaji ushindi.
“Kwa ambacho tumekipata ninaweza kusema kwamba wachezaji wanahitaji pongezi kwani walipambana na kuipa timu matokeo ambayo ilikuwa inahitaji kwenye mchezo wetu,” amesema.
Kwa sasa Yanga ipo kwenye maandalizi kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 6.