Home Habari za michezo BAADA YA KUTOA GUNDU KWA KUIFUNGA LIVER JUZI…MAN UTD WAZIDI KUTAKATA EPL…RONALDO...

BAADA YA KUTOA GUNDU KWA KUIFUNGA LIVER JUZI…MAN UTD WAZIDI KUTAKATA EPL…RONALDO APEWA MECHI YA MWISHO….


MANCHESTER United imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Southampton kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa St Mary’s.

Kwenye mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa bao la ushindi limefungwa na Bruno Fernades dakika ya 55.

Ni mashuti 17 ambayo Southampton walipiga huku matano yakilenga lango na United ni mashuti 11 walipiga huku 6 yakilenga lango.

Ushindi huo unaifanya United kufikisha pointi 6 baada ya kucheza mechi 4 ikiwa nafasi ya 6 na Southampton wenyewe wanabaki na pointi 4 nafasi ya 13 kwenye msimamo.

Bruno amesema ni furaha kwao kupata ushindi wakiwa ugenini jambo ambao walikuwa wanahitaji kuona linatokea.

“Tumefurahi kushinda mchezo wetu na ni furaha kwetu kwa jambo hili, pongezi kwa mashabiki namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi,” amesema.

Cr 7 alianza mchezo wa leo ambapo inatajwa kwamba ni mchezo wake wa mwisho kuwa na United kwa kuwa anahitaji kupata changamoto mpya.

Pia ingizo jipya Casemiro lilipata nafasi ya kuanza mchezo wa leo akitokea benchi dakika ya 80.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA SIMBA NA YANGA KAMA ZIMEMPOTEZEA HIVI...GEITA WAIBUKA NA HILI KUHUSU GEORGE MPOLE...