Home Habari za michezo FIFA KUUMULIKA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA KESHO….MWAMUZI WAO AKABIDHIWA RUNGU…

FIFA KUUMULIKA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA KESHO….MWAMUZI WAO AKABIDHIWA RUNGU…


Mwamuzi mwenye Beji ya FIFA, Elly Sasii anatarajia kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa dabi ya Kariakoo kati ya Yanga dhidi ya Simba utakaochezwa Agosti 13, Uwanja wa Mkapa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania iliweka wazi kuwa kwenye mchezo huo jumla ya waamuzi ambao watatumika ni watano mmoja kati wawili wasaidizi namba moja na namba mbili huku wawili wakiwa ni mwamuzi wa akiba na mtathimini waamuzi ambaye ni Nassor Hamdun (Kigoma).

Taarifa zinaeleza kuwa Sasii atakuwa kati wakati Mohammed Mkono kutoka Tanga atakuwa mwamuzi msaidizi namba moja na Kassi Mpango kutoka Dar es Salaam atakuwa mwamuzi msaidizi namba mbili.

Taarifa hiyo iliweka wazi jina la mwamuzi wa wa akiba kwenye mchezo huo kuwa ni Ramadhan Kayoko (Dar es Salaam).

Waamuzi wote hawa wanabeji za FIFA ambapo ni sawa na kusema kuwa FIFA wenyewe watakuwa wakiumulika mchezo huo mkubwa ambao utaashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku huo utakuwa ni mchezo wa nane kwa timu hizo kukutana tangu Ngao ya Jamii ilipoasisiwa mwaka 2001 Simba ikichukua mara nne, Yanga mara tatu.

SOMA NA HII  TETESI ZA USAJILI: BAADA YA KUONA MAMBO NI MAGUMU YANGA...MAKAMBO KUMFUATA ZAHERA....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here