Home Habari za michezo FT: POLISI TZ 2-1 YANGA SC….MAYELE ATUPIA KIMYA KIMYA….MWAMNYETO AOKOA CHAMA LA...

FT: POLISI TZ 2-1 YANGA SC….MAYELE ATUPIA KIMYA KIMYA….MWAMNYETO AOKOA CHAMA LA KIJANI….


Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Klabu ya Yanga imeanza vyema kampeni ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara 2022/2023 baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Wenyeji Polisi Tanzania ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Salum Kpemba baada ya makosa ya Nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto kuokoa mpira hovyo na kumgonga mfungaji dakika ya 35.

Dakika ya 41, Fiston Kalala Mayele akawarudisha Wananchi mchezoni baada ya kusawazisha goli dakika ya 41 na kufanya ubao usomeka 1-1, baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Polisi Tanzania.

Mpaka wanakwenda mapumziko bado matokeo yalibaki sare ya goli 1-1.

Kipindi cha pili Yanga walirudi kwa nguvu wakijaribu kusaka goli la ushindi na iliwabidi kusubiri mpaka dakika ya 85, Nahodha Mwamnyeto akimaliza krosi safi na kuihakikishia Yanga kuondoka na alama tatu.

SOMA NA HII  KISA BWALYA KUSEPA BONGO...STRAIKA KMC AIBUKA NA HILI...ATUMA MAOMBI MAZITO KWA SIMBA SC