Home Habari za michezo FT: TANZANIA 0-1 UGANDA… TAIFA STARS NJIA PANDA KUFUZU CHAN 2023….YAJICHONGEA NJIA...

FT: TANZANIA 0-1 UGANDA… TAIFA STARS NJIA PANDA KUFUZU CHAN 2023….YAJICHONGEA NJIA YA MOTO KAMPALA…


TIMU ya Taifa Stars imejiweka njia panda kufuzu Michuani ya Wachezaji wa ndani (CHAN) mashindano yatakayofanyika nchini Algeria 2023 baada ya kuchapwa bao 1-0 na Uganda mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa  jijini Dar es Salaam.

Akitokea benchi Mshambuliaji Travis Mutyaba aliwanyamazisha Watanzania waliohudhuria mechi hiyo dakika ya 87 baada ya kuchachafya ngome ya Taifa Stars.

Tanzania inahitaji kwenda kupindua meza mnamo tarehe 3 Septembar mwaka huu katika uwanja wa St.Mary nchini Uganda timu hizo zitarudiana

SOMA NA HII  KAZE MAMBO MENGINE YANUKIA IHEFU