Home Habar za Usajili Simba HUYU HAPA KIUNGO MKATA UMEME ANAYETAJWA KUTUA SIMBA…ANAKIPIGA TIMU YA TAIFA YA...

HUYU HAPA KIUNGO MKATA UMEME ANAYETAJWA KUTUA SIMBA…ANAKIPIGA TIMU YA TAIFA YA NIGERIA…ANABALAA HUYOOO…


MABOSI wa Simba SC, wamefikia makubaliano na kiungo mkabaji wa Rivers United, Morice Chukwu raia wa Nigeria, ambaye muda wowote atatambulishwa kikosini hapo kabla ya usajili kufungwa.

Kiungo huyo anatajwa kuwa ni pacha wa Nelson Okwa wakati wakiwa kwenye kikosi cha Rivers United, kabla ya Okwa hajajiunga na Simba hivi karibuni.

Simba chini ya kocha mkuu wa timu hiyo, Zoran Maki, imepanga kumtoa kwa mkopo kiungo mkabaji, Victor Akpan kurudi Coastal Union, ikiwa ni miezi michache tangu atambulishwe kikosini hapo.

Mpango wa Simba kumtoa Akpan ni kufuatia kiungo huyo kushindwa kuonesha kiwango bora mazoezini, hivyo Zoran akaomba aletewe kiungo mwingine mkabaji.


Taarifa za uhakika kutoka nchini Nigeria, zimebainisha kwamba, kila kitu juu ya usajili wa kiungo huyo kutua Simba kipo tayari.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Rivers United, kimesema kuwa, suala la Chukwu kutua Simba limekamilika kwa asilimia kubwa, kinachosubiriwa kwa sasa ni mchezaji huyo kumaliza majukumu ya timu ya taifa inayojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu CHAN dhidi ya Ghana.

“Ni kweli suala la Chukwu kwenda Simba lipo kwa asilimia kubwa kwa sababu tayari mchezaji, Simba na Rivers wameshakubaliana kila kitu.

“Nadhani wanachosubiri ni kumalizika kwa mchezo wa kuwania kufuzu CHAN kwa sababu kwa sasa yupo na timu ya taifa ya Nigeria akijiandaa na mchezo huo,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Rivers United, Charles Mayuku ambaye amelithibitishia gazeti hili kwa kusema: “Kweli hilo jambo lipo, lakini kwa sasa siwezi kuliongelea sana kwa sababu mchezaji mwenyewe ana majukumu ya kitaifa, baada ya mchezo huo kila kitu kitakuwa wazi juu ya uhamisho wake.”

SOMA NA HII  KISA 'MGOLI WA KIBABE' WA FEI TOTO DHIDI YA SIMBA....SHABIKI YANGA AFARIKI KWA KUZIDIWA NA FURAHA....