Home Habari za michezo KIPA LA KIMATAIFA ALIA KUKOSA NAFASI YA KUSAJILIWA YANGA….’ANG’ATA ULIMI’ KWA KAZE...

KIPA LA KIMATAIFA ALIA KUKOSA NAFASI YA KUSAJILIWA YANGA….’ANG’ATA ULIMI’ KWA KAZE NA NAMNA ALIVYOFUKUZWA…


Kipa mpya wa Geita Gold Mrundi, Arakaza MacArthur amesema alikaribia kujiunga na Yanga ila dili lake lilikwama baada ya, Cedric Kaze kutimuliwa.

Kaze aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga msimu wa 2020-2021, alitimuliwa pamoja na benchi lote la ufundi Machi 7, mwaka jana kufuatia matokeo mabovu.

Arakaza alisema wakati anaichezea Lusaka Dynamos ya Zambia alipigiwa simu na Kaze akimhitaji katika kikosi hicho kutokana na kuvutiwa na kiwango chake.

“Alinigharamia kila kitu kisha nikaanza safari ya Zambia hadi Dar es Salaam ila baada tu ya kufika naye akaachishwa kazi hivyo viongozi wa Yanga wakaniambia hawawezi kunisajili tena kwa sababu aliyehitaji huduma yangu anaondoka,” alisema na kuongeza;

“Niliumia sana kwa kweli kwa sababu kila mchezaji ana ndoto za kuchezea klabu kubwa ingawa ndio maisha ya mpira yalivyo, hivyo nikarudi Zambia, kabla ya kurudi tena Tanzania kujiunga na Geita Gold msimu huu ambayo ilionyesha nia ya dhati juu yangu, “ alisema.

Licha ya yote kumtokea Arakaza ila uongozi wa klabu hiyo ulimrejesha Kaze Septemba 24, mwaka jana akiwa msaidizi wa Nasreddine Nabi na ushirikiano wao umeifanya Yanga kucheza mechi 39 bila kupoteza, ikiwa ni rekodi mpya katika Ligi Kuu Bara tangu ilipoasisiwa mwaka 1965.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA SIMBA AVUNJA UKIMYA...AFUNGUKA NAMNA VIONGOZI 'WANAVYOMHENDO'...AANIKA MAKUBALIANO YOTE...