Home Habari za michezo KIPIGO CHA 4-0 KUTOKA BRIGHTON CHAWAINUA MASHABIKI MAN UTD…WIBUKA NA MSIMAMO HUU...

KIPIGO CHA 4-0 KUTOKA BRIGHTON CHAWAINUA MASHABIKI MAN UTD…WIBUKA NA MSIMAMO HUU MKALI KWA WENYE TIMU…


THE Manchester United Supporters’ Trust (MUST) imetaka majibu kutoka kwa familia ya Glazer kuelezea kwanini klabu hiyo imeanza na matokeo mabaya na yakufedhehesha.

United wako mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kufungwa na Brighton siku ya Jumamosi kwa bao 4-0.

Taarifa iliyoandikwa na kundi hilo ilisomeka: “Kwa kawaida huwa hatutoi maoni kuhusu masuala ya uwanjani, lakini tuliona kwamba tunapaswa kufanya hivyo katika hafla hii.

Baada ya kupata aibu na matokeo mabovu msimu uliopita, na bado mpaka sasa kumedhorota kwa dirisha la usajili, matumaini hayakuwa makubwa kabisa kuingia katika msimu huu. Lakini hatufikirii watu wengi walitarajia mambo kuwa mabaya ya kufedhehesha kama ilivyokuwa Jumamosi jioni.

Ujumbe huo uliendelea kwa kusema “Kama tulivyosema siku zote, samaki huoza kichwani. Na jukumu la mwisho la hali mbaya ya klabu yetu lazima liwe juu wamiliki wake, familia ya Glazer.

Sasa ni kwao kuwaeleza mashabiki wa United kwa nini wako katika hali hii, na watafanya nini kuihusu suala hili. Tumekuwa na nyakati ngumu katika muongo mmoja uliopita, lakini hii inahisi kuwa chini kabisa. “Kama tulivyosema kwenye taarifa yetu Jumamosi usiku, sisi kama mashabiki tunatakiwa kushikamana.

Umoja ni nguvu na sauti moja ya umoja inayoelekezwa kwa klabu na wamiliki inahitajika zaidi kuliko hapo awali.” Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

SOMA NA HII  BUMBULI : SIMBA WANA ROHO MBAYA....HAWAZUNGUMZI CHOCHOTE...WANAONA TUTAPATA PESA NYINGI...