Home Geita Gold FC KISA GEORGE MPOLE…GEITA GOLD WASUASUA KUWEKA KAMBI YA MAAMNDALIZI YA LIGI…UONGOZI WAVUNJA...

KISA GEORGE MPOLE…GEITA GOLD WASUASUA KUWEKA KAMBI YA MAAMNDALIZI YA LIGI…UONGOZI WAVUNJA UKIMYA….


Nyota watatu wa Geita Gold waliopo timu ya taifa ‘Taifa Stars’ George Mpole, Danny Lyanga na Kelvin Nashon wameichelewesha safari ya kambi itakayokuwa Burundi kujiandaa na msimu ujao wa mashindano.

Wachezaji hao ni sehemu ya kikosi cha Stars kinachoshuka uwanjani leo kuvaana na Somalia katika mechi ya kuwani kufuzu Fainali za Chan na baada ya mchezo huo kesho wataungana na wenzao kwa safari ya Burundi.

Akizungumza Mwenyekiti wa Geita Gold, George Biligenda alisema timu imeingia kambini kuanza mazoezi, lakini imeshindwa kuondoka kwa sababu ya nyota hao.

Alisema wakiwa Burundi watakaa kwa siku 14 kabla ya kurejea nchini kuanza Ligi Kuu Agosti 17 sambamba na michuano ya CAF itakayoanza mapema Septemba.

“Timu imeshaanza maandalizi ya awali kabla ya safari wachezaji walio timu ya taifa mara baada ya mchezo wao, Jumapili na Jumatatu tunaanza safari kwenda Burundi,” alisema Biligenda. “Tumeamua kuweka kambi Burundi baada ya kubaini kuwa tutakuwa na uwezo wa kupata timu nyingi za kucheza nazo mechi za kirafiki na zitakuwa kipimo kizuri”

SOMA NA HII  AHMED ALLY AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU VIINGILIO VYA SIMBA DAY MAMBO HADHARANI