Home Habari za michezo KUELEKEA DK ZA MWISHO ZA USAJILI KUFUNGWA TZ….SINGIDA BS WAIVURUGA SIMBA KWA...

KUELEKEA DK ZA MWISHO ZA USAJILI KUFUNGWA TZ….SINGIDA BS WAIVURUGA SIMBA KWA ONYANGO…ISHU YOTE NZIMA IKO HIVI…


SIMBA usiku wa juzi ilikuwa uwanjani kumalizana na Asante Kotoko na itapumzika kwa siku mbili kabla ya kuivaa Al Hilal Sudan katika mechi za kirafiki za kimataifa zilizoandaliwa na Wasudani, lakini taarifa iwafikie mashabiki wa klabu hiyo kuwa beki kisiki Joash Onyango anang’olewa kikosini hapo.

Kikosi cha Simba kipo Sudan kwenye mechi hizo mbili za kirafiki za kimataifa zilizoandaliwa na Al Hilal kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa michuano za CAF inayoanza mwezi ujao, lakini kiliondoka nchini wikiendi iliyopita bila Onyango baada ya beki huyo Mkenya kugoma kuondoka.

Sasa inaelezwa kabla ya Simba kurudi nchini kutoka Sudan mabosi wa klabu hiyo wanatarajia kukutana ili kumjadili mchezaji huyo, lakini kukiwa na taarifa kwamba huenda akang’oka klabu hapo kutokana na kupata dili jipya kutoka uongozi wa timu ya Singida Big Stars wanaotaka kumsajili.

Taarifazinasema kwamba mabosi wenye uamuzi wa Singida wamefanya mazungumzo mazito kwa pamoja na Onyango na kumueleza wapo tayari kumchukua.

Mabosi hao baada ya kuzungumza na Onyango walimueleza kama atafanikiwa kupata barua kutoka Simba ya kusitisha mkataba wake kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatano wiki hii, basi watamsainisha mkataba wa miaka miwili kwa maslahi waliyokubaliana kupitia mazungumzo hayo.

Kwa kujua tayari imeshatimiza idadi ya wachezaji 12 wa kigeni kwa sasa na hasa baada ya kushusha kiungo mshambuliaji kutoka Argentina, Miguel Escobar, mabosi hao wamepanga kama watamchukua Onyango basi watamuachia mchezaji mmoja wa kigeni aliyepo kikosini ili kuepuka matatizo na TFF.

Taarifa hiyo inaeleza mabosi wa Singida wamefikia hatua hadi ya kuongea na Onyango kutokana na msukumo walioupata kutoka kwa nahodha wao, Pascal Wawa aliyewaeleza kama atapatikana beki huyo basi ukuta wa chuma utakuwa umekamilika.

Wawa aliyewahi kucheza pamoja na Onyango kwa misimu miwili mfululizo ndani ya Simba amewaambia mabosi wake kuhakikisha wanapambana kama kutakuwa na uwezekano wa kumpata beki huyo wahakikishe wanamchukua haraka iwezekanavyo.atika kuhakikisha suala la Onyango linapewa nafasi kubwa ndani ya Singida, Wawa hakuishia hapo alikwenda kumshawishi hadi kocha wa timu hiyo, Hans Pluijm ambaye naye ametoa ruhusa kwa mabosi kama watafanikiwa kumpata litakuwa jambo zuri kutokana na ubora wake.

SOMA NA HII  BAADA YA MASHABIKI WA SIMBA KULIA KWAMBA 'WANAOUMIA NI WAO'...TRY AGAIN AIBUKA NA KUWAJIBU HIVI.....

Baada ya mazungumzo ya usiri mkubwa kati ya Wawa, Onyango na mabosi wenye uamuzi Singida Big Stars walimueleza mchezaji huyo apambane kama ataweza kuvunja mkataba wake Simba anasainiwa siku hiyohiyo.

Upande wa viongozi Simba wakiendelea kutafakari suala la mchezaji kugoma kwenda Sudan kutokana na sababu alizoweka wazi, Onyango ameendelea kupambana kuomba avunjiwe mkataba wake kama atashindwa kutimiziwa ahadi zake katika mkataba mpya licha ya kupewa uhakika wa kucheza mara kwa mara kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Inafahamika kwamba baada ya viongozi wa Simba kufahamu kuna dili hilo la Onyango kutakiwa Singida ndio maana analazimisha kuvunjiwa mkataba, wanaweza kumuwekea ngumu na wakabaki naye hadi dirisha la usajili litakapofungwa Agosti 31.

Hakuna kiongozi yeyote wa Simba au Singida aliyepatikana jana kuzungumzia juu ya suala hilo la Onyango aliyesajiliwa msimu wa 2019-2020 akitokea Gor Mahia ya nchini kwao, Kenya.