Home Habari za michezo KUELEKEA KESHO SIKU YA WANANCHI….PITSO MOSIMANE AIPA UJIKO YANGA…AAMUA KUPUMZIKA SOKA…

KUELEKEA KESHO SIKU YA WANANCHI….PITSO MOSIMANE AIPA UJIKO YANGA…AAMUA KUPUMZIKA SOKA…


Aliyekuwa Kocha Mkuu wa miamba ya Soka Barani Afrika, Al Ahly ya Misri, Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini amesema baada ya kutumika kama kocha kwa miaka 21, sasa ameamua kupumzika ili kufanya mambo mengine nje ya ukocha.

Pitso amesema hayo leo Ijumaa, Agosti 5, 2022 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam baada ya kukaribishwa na Klabu ya Yanga katika tamasha la Kilele cha Wiki ya Wananchi litakalofanyika kesho katika Dimba la Mkapa.

“Nikiwa kama Kocha kutoka Afrika nimefanya makubwa kwenye soka la Afrika na nina amini Afrika tuna nafasi ya kufanya zaidi ya nikichokifanya kwenye soka kukuza mpira wetu Ulimwenguni kote.

“Nilikuwa Uwanjani kila siku na mechi za mashindano zikiwa kila baada ya siku 3 na nilikuwa nasafiri sana, sasa nimeamua kupumzika na mapumziko yangu nayatumia kushiriki na Young Africans SC katika Wiki ya Wananchi,” amesema Pitso.

SOMA NA HII  DILI LA MSUVA KUTUA YANGA SI MCHEZO AISEE...GSM WAMWEKEA MEZANI MIL 350...NABI APAGAWA KWA MAVITU YAKE...