Home Habari za michezo KUELEKEA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA MSIMU HUU…YANGA WAPANGUA MTEGO WA CAF...

KUELEKEA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA MSIMU HUU…YANGA WAPANGUA MTEGO WA CAF MAPEMA….KAZI IMEBAKI HAPA…


Majina ya wachezaji 27 klabu ya Yanga ambao watashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayoandaliwa na shirikisho la soka barani Afrika (CAF) yamewasilishwa kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki kabla ya kipute cha michuano kurejea tena.

Yanga ambao ndiyo Mabingwa wa Soka Tanzania Bara watashiriki michuano hiyo sawa na wapinzani wao wa karibu Simba SC ambapo zote kwa pamoja zitaanza hatua ya awali.

Kuwasilisha majina hayo mapema ni sawa na kukwepa mtego wa anguko la msimu uliopita kwani majina yalichelewa kupelekwa CAF jambo lililosababisha kuwakosa baadhi ya wachezaji muhimu kwenye mechi za awali.

Wakati Simba na Young Africans zinaiwakilisha Tanzania kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Geita Gold FC zikishiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Majina ya Wachezaji wote watano wa Kigeni waliosajiliwa Klabuni hapo Stephen Aziz Ki, Bernard Morrison, Lazarius Kambole, Joyce Lomalisa na Gael Bigirimana yapo kwenye orodha hiyo.

Young Africans itaanza kupambana Kimataifa kwa kuwakabili Mabingwa wa Soka Sudan Kusini Zalan FC itakayokua nyumbani katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza kati ya Septemba 9 -11.

Orodha ya majina wa Young Africans iliyowasilishwa ‘CAF’ ni:-

Magolikipa:- Djigui Diara, Abutwalib Msheri na Erick Johora.

Mabeki:- Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Joyce Lomalisa, David Bryson, Djuma Shaban, Abdalla Shaib, Yanick Bangala pamoja na Shomari Kibwana.

Viungo: Abubalar Salum, Zawadi Mauya, Crispin Ngushi, Dickson Ambundo, Gael Bigirimana, Khalid Aucho, Jesus Moloko, Feisal Salum, Yusuph Athuman, Bernard Morrison, Denis Nkane, na Farid Mussa.

Washambuliaji: Lazarius Kambole, Fiston Mayele, Stephan Aziz Ki, na Heritier Makambo

SOMA NA HII  MAN CITY, CHELSEA MAMBO SIO MAMBO TENA