Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA KUTEMWA SIMBA….KAPAMA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA A-Z KUTOONEKANA KAMBINI…

KUHUSU ISHU YA KUTEMWA SIMBA….KAPAMA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA A-Z KUTOONEKANA KAMBINI…


Kiungo wa Simba, Nassoro Kapama hakuwepo katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Jumapili asubuhi siku moja baada ya kikosi hicho kutoka kucheza mechi dhidi ya Kagera Sugar na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kumekuwa na taarifa nyingi za kuhusu kiungo huyo kuondoka Simba kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha timu hiyo tangu kimerejea nchini kutokea Misri.

Alipoulizwa Kapama amesema alishindwa kwenda mazoezi kutokana na sababu za kifamilia zilizokuwa nje ya uwezo wake hadi kushindwa kuwepo katika awamu hiyo moja ya mazoezi.

Kapama amesema hakuna suala lolote kuhusu kuondoka Simba na hayo masuala mengine ni mambo ya kifamilia ambayo yanaendelea katika mitandao ya kijamii.

“Nipo kwenye timu na naendelea ratiba zote za timu kama ilivyo kawaida nilishindwa kuwepo kutokana katika mazoezi kutokana na mambo hayo ya kifamilia yakimalizika nitakuwepo kama kawaida,” amesema Kapama.

SOMA NA HII  NABI ASHUSHA MAJEMBE MAPYA YANGA..MKUDE, AJIBU WAPENYA KIKOSI CHA KOCHA MPYA SIMBA...SPOTI XTRA