Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA MATOLA KUIHUJUMU SIMBA DHIDI YA YANGA…UONGOZI WATOA TAMKO HILI...

KUHUSU ISHU YA MATOLA KUIHUJUMU SIMBA DHIDI YA YANGA…UONGOZI WATOA TAMKO HILI RASMI…


Baadhi ya Mashabiki wa Simba SC wamekua wakilaumu maamuzi ya Uongozi wa Klabu hiyo kushindwa kumuondoa Matola kila unapomfukuza Kocha Mkuu, kwa madai amekua akifanya hujuma kupitia wachezaji.

Ahmed Ally amesema lawama anazotupiwa Kocha Matola hazina maana katika kipindi hiki na badala yake anapaswa kuchukuliwa kwama mtendaji mzuri katika Benchi la Ufundi kama ilivyo kwa watendaji wengine.

Amesema lawama za kutaka Kocha huyo mzawa kuondolewa katika majukumu yake, hasa Simba SC inapopoteza mchezo dhidi ya Young Africans, ni kutokufahamu vizuri matokeo ya mchezo wa soka kwa Mashabiki ambao wamekua wakitumia hiyo kama sababu.

“Hizo lawama unazozisikia kuhusu Matola na kocha Zoran zimetokana na hakuna anayeamini kama tumefungwa. Huu ndiyo mpira unaweza usifanye makosa na ukaadhibiwa.”

“Mashabiki wanapaswa kujua safari hii tuna timu nzuri sana, Yes Yanga wana timu nzuri, lakini hawana timu nzuri ya kutuzidi sisi” amesema Ahmed Ally

SOMA NA HII  IMETIKI.....BAADA YA KUSUSWA NA TIMU ZA BONGO....KABWILI APATA TIMU RWANDA....MCHONGO MZIMA KAZE ANAUJUA...