Home Habari za michezo LICHA YA KUWA HAYUPO….BARBARA AFUNGUKA NAMNA WANAVYOTEMBEA NA MIPANGO, MAWAZO YA PABLO…

LICHA YA KUWA HAYUPO….BARBARA AFUNGUKA NAMNA WANAVYOTEMBEA NA MIPANGO, MAWAZO YA PABLO…

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa ripoti ya usajili amayo inatumika kwa sasa ni ileiliyoachwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Pablo Franco raia wa Hispania.

Pablo alikuwa ndani ya Simba msimu wa 2021/22 alipobeba mikoba ya Didier Gomes alichimbishwa hapo baada ya kushindwa kutimiza makubaliano yalikuwa kwenye mkataba na mchezo wake wa mwisho ilikuwa ni Mei 28.

Katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mtupiaji akiwa ni Feisal Salum aliyemtungua Aishi Manula kwa pasi ya Salum Aboubhakari,’Sure Boy’.

Barbara Gonzalez,Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa wanatumia ripoti ya Pablo kufanya usajili pamoja na kushauriana na kocha mpya wa sasa ambaye ni Zoran Maki.

“Katika usajili ambao tunafanya tunatumia ripoti ya Pablo,(Franco) ambaye alitupatia pamoja na kuangalia pale ambapo kulikuwa na mapungufu kwa kushirikiana na kocha wa sasa,(Maki) ili kuwa na timu imara zaidi,” .

Tayari Simba imewatambulisha wazawa wawili ambao ni Nassoro Kapama na Habib Kyombo wengine ambao ni wachezaji wakigeni ni Victor Ackpan,Moses Phiri na Augustino Okra pia mwingine ni Nelson Okwa.

Imeachana na mastaa watatu ambao walikuwa kambini pia nchini Misri ambaye ni Chris Mugalu,Meddie Kagere na Taddeo Lwanga.

SOMA NA HII  NYOTA WAPYA MTIBWA SUGAR WAWEKA WAZI MALENGO YAO