Home Burudani MALUE LUE YA KIFO YAZIDI KUMVURUGA TYSON…AANZA KUOMBA MSAMAHA ALIOWAKOSEA,…AFUNGUKA ISHU YAKE...

MALUE LUE YA KIFO YAZIDI KUMVURUGA TYSON…AANZA KUOMBA MSAMAHA ALIOWAKOSEA,…AFUNGUKA ISHU YAKE NA EVANDER..


Mike Tyson; ni bondia maarufu mstaafu wa Marekani ambaye anasema kuwa, kuna matukio mengi anayakumbuka kwenye maisha yake, lakini kubwa anajutia kumng’ata sikio bondoa mwenzake, Evander Holyfield, tukio ambalo alilifanya Novemba 9, 1996.

Tyson anasema; “Ikiwa unaona au kuhisi kuna sauti inakutesa katika maisha yako, usijihukumu, bado una muda wa kuifuta na kujirekebisha pale ulipokosea.

“Kuna mambo mengi ninayoshukuru. Hata hivyo, kuna mambo mengi niliyotenda nyuma nikiyatazama najuta.

“Tukio maarufu la kuuma sikio ni tukio ambalo lingenitesa katika maisha yangu yote.

“Ninashukuru kwa dhati kwamba nilipata fursa ya kurekebisha matendo yangu na kwamba Evander alikuwa mwenye neema ya kutosha kunisamehe. “Ninamheshimu sana na nina furaha kwamba urithi wetu kama binadamu si lazima uelezewe katika wakati huu mgumu.”

Tyson mwenye umri wa miaka 66 anadaiwa kuwa kwenye hali mbaya kiafya na amekuwa akiwaomba msamaha watu wote aliowakosea akidai kuona kifo chake kipo karibu.

SOMA NA HII  KASI YA BENCHIKHA YAWASHITUA MAKOCHA