Home Habari za michezo MKATABA MPYA NA M-BET….TRY AGAIN AFUNGUKA WALIVYO’BUSTIWA’ NA ‘KISHIKA UCHUMBA’ CHA MIL...

MKATABA MPYA NA M-BET….TRY AGAIN AFUNGUKA WALIVYO’BUSTIWA’ NA ‘KISHIKA UCHUMBA’ CHA MIL 400….


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amefichua siri ya usajili wao msimu huu akisema kwa sehemu kubwa umechangiwa na wadhamini wao wapya.

Try Again amesema wakiwa kwenye maandalizi ya msimu huu mpya wapewa fungu ambalo wamelitumia kwenye usajili wao.

“Tumepewa Sh400 milioni kabla ya kusaini mkataba huu, zimetumika kwenye usajili wetu ambao umefanyika,” amesema Try Again.

Try Again amesema kwenye upande wa udhamini watahakikisha wanasimamia vizuri fedha hizo na kutumika ipasavyo.

“Fedha ni nyingi na sisi bodi tutahakikisha tunasimamia juu ya fedha hizo, tutaheshimu mkataba,” amesema Try Again.

Try Again amesema wanawashukuru wadhamini wao wa zamani kwani ndani ya miaka mitano walikuwa na mafanikio makubwa.

“Lazima tuwe na shukrani na mdhamini wetu wa zamani kwani tulikuwa na mafanikio na ndio maana leo M-Bet imeingia,” amesema Try Again.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA KUMSAJILI BOBOSI NA MANZOKI...SIMBA SC WAANIKA UKWELI ULIVYO...