Home Habari za michezo PAMOJA NA KUSAJILIWA YANGA…AZIZ KI ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA IVORY COAST…MCHEZAJI...

PAMOJA NA KUSAJILIWA YANGA…AZIZ KI ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA IVORY COAST…MCHEZAJI WA AZAM NAYE AULA…


KIUNGO mpya wa Yanga, Stephane Aziz Ki ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi ya Ivory Coast kwa msimu uliopita wakati akiichezea Asec Mimosas.

Nyota huyo ambaye amejiunga na Yanga msimu huu usajili wake ulikuwa gumzo kutokana na utambulisho wake uliofanyika Julai 15 alfajiri huku akitegemewa kufanya makubwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara kwa sababu ya kiwango chake kizuri ambacho alionyesha.

Mbali na Aziz Ki ila kiungo mpya wa Azam FC, Tape Edinho ameshinda pia tuzo ya kiungo bora wa msimu wakati akiitumikia klabu ya ES Bafing FC ya kwao Ivory Coast.

Katika tuzo hizo za msimu, Edinho alimshinda nyota wenzake wa Azam, Kipre Junior aliyesajiliwa naye msimu huu akitokea Sol FC ya huko huko Ivory Coast sambamba na nyota mwingine, Djire Abdoulaye anayechezea klabu ya Racing Club Abidjan.

SOMA NA HII  YANGA WAONA ISIWE TABU WAMALIZANA KIMYAKIMYA NA BIGIRIMANA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here