Home Habari za michezo SAKATA LA KUTOLEWA KWA MKOPO….AKPAN AJIFANYA HAJUI KINACHOENDELEA SIMBA….AJITETEA NA KAMBI YA...

SAKATA LA KUTOLEWA KWA MKOPO….AKPAN AJIFANYA HAJUI KINACHOENDELEA SIMBA….AJITETEA NA KAMBI YA MISRI…


Kiungo mpya wa Simba, Victor Akpan anayetajwa kutakiwa kutolewa kwa mkopo Coastal Union, amesema hajui lolote juu ya dili hilo linaloelezwa kufanywa kwa sababu ya kocha Zoran Maki kutokubali kiwango chake tangu awe naye kambini Misri.

Akizungumza kiungo huyo mkabaji kutoka Nigeria alisema hajui lolote juu ya dili la mkopo kwa vile hajaelezwa na viongozi wala kocha. “Sijui kama nataka kutolewa kwa mkopo. Ujue nimesajiliwa hivi karibuni na nilikuwa kambini tangu timu ikiwa Misri.

“Kama jambo hilo lipo basi ni wewe (mwandishi) unayenieleza,” alisema Akpan aliyeisaidia na wenzake Coastal kufika fainali ya ASFC na kulala kwa Yanga.

Alipoulizwa kama yupo tayari kurudi Coastal, alisema ni mapema kwake kusema lolote.

SOMA NA HII  MAYELE ATUPA JIWE GIZANI BAADA YA AZAM KUPOKEA KIPIGO DHIDI YA YANGA