Home Habari za michezo SIMBA, YANGA NA AZAM ZAPEWA KAMSELELEKO MICHUANO YA CAF…MBINU ZOTE ZA USHINDI...

SIMBA, YANGA NA AZAM ZAPEWA KAMSELELEKO MICHUANO YA CAF…MBINU ZOTE ZA USHINDI SASA WAZI…MAKI AONYWA…


Zimebaki takribani wiki mbili, klabu ya wawakilishi wa Tanzania kuanza kutupa karata kwenye michuano ya CAF, jambo lililowaibua mafaza wa Simba na Yanga ambao wamewalainishia kazi nyota wa klabu hiyo sambamba na Geita Gold na Azam ili watoboe kwenye mechi hizo za kimataifa.

Yanga itatupa karata yake dhidi ya Zalan ya Sudan Kusini, huku Simba ikipepetana na Nyasa Big Bullets ya Malawi katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Geita itacheza na Hilal Alsahil ya Sudan katika Kombe la Shirikisho ikianza raundi ya awali, huku Azam itaanzia raundi ya kwanza.

Mechi za mkondo wa kwanza kwa raundi ya awali zitapigwa kati ya Sept 9-11 na kurudiana wiki moja baada na mastaa wa zamani nchini wametoa ushauri kwa nyota wa timu hizo wakiwamo Stephane Aziz KI, Bernard Morrison, Augustine Okrah, Nelson Okwa na Kipre Jr pamoja na Tepsie Evance wa Azam kwamba kuanza mapema kujiweka vyema kisaikolojia ili wazifikishe timu hizo mbali.

Kipa wa zamani wa Yanga, Benjamin Haule alisema; “Morali ikiwa juu itawajengea kujiamini ambako kutakuwa na uwezekano wa kuzalisha mabao mengi, mfano wamewaongeza Bernard Morrison, Aziz Ki, Joyce Lomalisa ambao ni wazoefu na watawaongezea nguvu kina Fiston Mayele, Yanick Bangala na wengine.

“Simba ipo kipindi cha mpito, kocha ana kazi ngumu kutengeneza kombinesheni, lakini uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kama kina Okrah, Okwa, Phiri (Moses) unaonekana na huo unapaswa kutumika kipindi hiki kilichopo kama changamoto na jambo la msingi wajitambue na kuwajibika.”

Nyota wa zamani wa kimataifa aliyekipiga klabu hizo kongwe na Taifa Stars, Amir Maftah alisema; “Hata kama timu wanazoanza nazo hazina rekodi kali za ushindani, ili mradi zinacheza michuano ya CAF wasizipuuze, kama wataweza kuzifunga mabao mengi watumia nafasi hiyo kufanya hivyo, ninachosisitiza waachane na mpira wa shoo wanapokuwa wapo mbele kwa mabao, wanapaswa kupambana mwanzo, mwisho kazi ya kushangilia sana ni ya mashabiki,” alisema Maftah, huku kocha Kennedy Mwaisabula, akisema timu hizo zina uzoefu wa kucheza kimataifa, hivyo wanapaswa kujiandaa kulingana na majukumu yaliyopo mbele yao.

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGWA NA WATUNISIA....KIGOGO YANGA ASHINDWA KUJIZUIA...KAFUNGUKA YA NDANI...

“Jambo la msingi waongeze umakini, maana kosa moja tu litaigharimu timu, lazima watulie kwa faida ya timu.”