Home Habari za michezo WAKATI TAARIFA ZA ‘VIJIWENI’ ZIKISEMA KOCHA SIMBA ANAWACHUKIA CHAMA NA PHIRI…KUMBE...

WAKATI TAARIFA ZA ‘VIJIWENI’ ZIKISEMA KOCHA SIMBA ANAWACHUKIA CHAMA NA PHIRI…KUMBE UKWELI WA MAMBO UKO HIVI…


Kocha Mkuu wa Simba, Zoran Maki, ameufurahia muunganiko wake wa safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Clatous Chama, Augustine Okrah na Moses Phiri huku akisema kuwa licha ya kutocheza kwa muda mrefu wakiwa pamoja lakini kuna matunda makubwa yanaanza kuonekana walipocheza pamoja.

Okrah na Phiri wote kwa pamoja ni maingizo mapya katika kikosi cha Simba huku Chama yeye akiwa mzoefu ndani ya kikosi hicho, japo wote wakicheza kwa maelewano makubwa ambapo wote wamefanikiwa kuifungia Simba katika michezo miwili ya ligi iliyopita.

Kocha Maki alisema kuwa amefurahi kuona muunganiko mzuri wa washambuliaji hao ambao kwa pamoja licha ya kutocheza kwa muda mrefu lakini kuna maelewano mazuri ambayo yamesababisha timu kupata ushindi huku akiamini kuwa huko mbeleni wakizoeana vizuri basi wataipatia Simba mafanikio makubwa sana.

“Ni wachezaji ambao wameonyesha kuwa na muunganiko mzuri na maelewano mazuri licha ya kucheza kwa muda mfupi kwa pamoja ndani ya Simba, naamini wakikaa kwa pamoja, kuna muunganiko mkubwa tutaupata kutoka kwao, tayari unaona kila mmoja amefunga na kutengeneza nafasi nzuri na mimi ndio jambo ninalolihitaji kutoka kwao kwa manufaa ya timu,” alisema kocha huyo.

SOMA NA HII  UNAAMBIWA KISA ULE USHINDI NA SOKA SAFI LA AZAM FC JUZI...NABI AZIDI 'KUDATA' HUKOO...KATOA MBINU ZOTE....