Home Habari za michezo WAKIJUA WATACHEZA NA SIMBA HIVI KARIBUNI…KMC WAANZA MBWEMWE HIZI ZA HATARI…WAPANGA...

WAKIJUA WATACHEZA NA SIMBA HIVI KARIBUNI…KMC WAANZA MBWEMWE HIZI ZA HATARI…WAPANGA KUJA KWA STAILI MPYA…


Wakijiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Simba, timu ya KMC imerejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ambao utapigwa Septemba 7 mwaka huu.

Kikosi cha KMC ambacho kilikuwa jijini Arusha kwa ajili ya mechi mbili za Ligi dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union kimeambulia pointi moja baada ya kupooteza mchezo wa kwanza.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa:

β€œTimu ilirejea Dar Jumatatu na kutoa mapumziko ya siku moja kwa wachezaji ambapo juzi Jumanne kiliingia kambini na kuanza kwa program ya gym na leo hii asubuhi kuendelea na mazoezi ya kawaida ya uwanjani.

β€œKatika kipindi hiki cha mapumziko tutakuwa na program mbalimbali ikiwemo kucheza mechi za kirafiki ambapo kesho tutakuwa ugenini dhidi ya As Arta Solar 7 kutoka nchini Djibout mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru, Dar.

β€œKwa kipindi hiki ambacho tupo kwenye mapumziko, tunahitaji mechi nyingi za kirafiki kadri ambavyo tutazipata, na tayari tumepata mechi moja ambayo tutacheza kesho lengo ni kufanya maboresho ambayo yataiwezesha Timu kufanya vizuri zaidi katika michezo inayokuja.β€œ

SOMA NA HII  KISA MECHI NA KMC....YANGA WAINGIA 'BARIDI' WABADILI GIA ANGANI..ISHU NZIMA IKO HIVI