Home Habari za michezo A-Z JINSI MKUU WA MKOA DAR ALIVYOOKOA UJENZI UWANJA WA SIMBA…APIGA BITI...

A-Z JINSI MKUU WA MKOA DAR ALIVYOOKOA UJENZI UWANJA WA SIMBA…APIGA BITI LA KUBOMOA NDANI YA SIKU 60…


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla leo Jumatano (Septemba 14) amemaliza mgogoro wa Ardhi katika kiwanja namba 229 Kinachomilikiwa na Simba SC maeneo ya Bunju B Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

RC Makalla baada ya kuzuru eneo la kiwanja alipata wasaa wa kujionea mipaka na Wananchi takribani 9 ambao wamevamia na kujenga katika eneo hilo.

Aidha RC Makalla amewataka wananchi waliovamia katika kiwanja hicho ndani ya siku 60 kuanzia leo Jumatano (Septemba 14) kujipanga kuondoka mara moja kwa kuwa eneo hilo ni mali halali ya Simba SC ndio wenye hati miliki.

“Uvamizi wa Ardhi ni ualifu kama ulivyo ualifu mwingine wowote ambapo anayetenda kosa anastahili kuchuliwa hatua za kisheria” Amesema RC Makalla

RC Makala walipokua akikagua sehemu ya eneo la Uwanja wa Simba Bunju B, Dar es salaam

Katika hatua nyingine RC Makalla ameelekeza Uongozi wa Simba SC kuanza mara moja ujenzi wa uzio kuzunguka kiwanja hicho kama walivyokusudia huku akimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe amemuagiza OCD kusimamia Ulinzi na Usalama katika eneo hilo katika Kipindi chote cha Utekelezaji wa zoezi hilo.

Hata hivyo RC Makalla ametoa Rai kwa Simba SC kuendeleza uwekezaji wa kiwanja hicho kwa kuwa ni fursa ya kibiashara kwa wakazi wa Bunju Wilaya, Mkoa na Taifa kwa Ujumla.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIMUALIKA KINANA....SIMBA WAMUALIKA RAIS WA CAF KWENYE SIMBA DAY...KARIA WA TFF ATOA TAMKO...