Home Habari za michezo BAADA YA ‘KUBONDWA’ NA ZAMBIA JUZI….TWIGA STARS WARUDI KWA HASIRA…’WAIFUMUA’ MALAWI BILA...

BAADA YA ‘KUBONDWA’ NA ZAMBIA JUZI….TWIGA STARS WARUDI KWA HASIRA…’WAIFUMUA’ MALAWI BILA HURUMA…


Baada ya kupata maumivu ya kupokonywa ubingwa na Zambia kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Cosafa, hatimaye timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ imejifuta machozi ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namibia na kumaliza nafasi ya tatu.

Katika michuano hiyo inayoendelea nchini Afrika ya Kusini, Tanzania ilishiriki kama bingwa mtetezi baada ya kulichukua taji hilo mwaka jana.

Mchezo huo ambao ulianza saa 7:00 mchana kwa saa za Tanzania ndiyo ilikuwa yakwanza kuandika bao kupitia mkwaju wa faulo iliyopigwa na Christer Bahera dakika ya 12 kabla ya Aisha Juma kuisawazishia Namibia kwa kujifunga mwenyewe dakika ya 20, wakati anajaribu kuokoa mpira wa krosi iliyopigwa na Zenatha Coleman na kufanya kipindi cha kwanza kimalizike

Mabadiliko ya kipindi chapili kuingia kwa Enekia Kasonga, Mwanahamisi Omary na Diana Msewa yalichangia kuongeza kasi kwenye eneo la ushambuliaji la Twiga na dakika ya 88, krosi iliyopigwa na Mwanahamisi ilitua kwenye boksi la Namibia na katika harakati za kuokoa kapteni Emma Naris akajikuta anaweza mpira nyavuni na kuipa Tanzania uongozi ambao ulidumu hadi mchezo unamalizika.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO