Home Habari za michezo BAADA YA KUFANYA KAZI NZURI TOKA KUANZA KWA MSIMU…CHAMA AKABIDHIWA UFALME SIMBA…MASHABIKI...

BAADA YA KUFANYA KAZI NZURI TOKA KUANZA KWA MSIMU…CHAMA AKABIDHIWA UFALME SIMBA…MASHABIKI WAMPITISHA….

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month) wa Simba SC kwa mwezi Agosti, 2022.

Chama ametangazwa mshindi wa tuzo hiyo, baada ya kuwashinda kwa Kura viungo wenzake Pape Sakho (Senegal) na Sadio Kanoute (Mali) ambao aliingianao Fainali kwenye kinyang’anyiro hicho.

Majina ya wachezaji hao yalianikwa hadharani kupitia kurasa za Mitandao ya Simba SC, na Mashabiki wa klabu hiyo walipiga kura kupitia tovuti ya klabu kuanzia Agosti 29 hadi Septemba Mosi.

Chama ameongoza kwa kupata kura 1551 sawa na asilimia 60.30, Kanoute alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 516 sawa na asilimia 20.06 na Sakho alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 506 sawa na asilimia 19.63.

Kwa ushindi huo, Chama atakabidhiwa Fedha taslimu Shilingi 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

Kwa mwezi Agosti Chama amecheza michezo yote tatu sawa na dakika 231 akifunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa mengine matatu.

SOMA NA HII  KWA TAARIFA YAKO....HIZI HAPA NDIO TIMU RASMI ZITAKAZOSHIRIKI MICHUANO MIPYA YA CAF SUPER LEAGUE....