Home Habari za michezo BAADA YA KUKIANGALIA KIKOSI CHA SIMBA…MGUNDA KAFUNGA MACHO KISHA AKASEMA HILI KWA...

BAADA YA KUKIANGALIA KIKOSI CHA SIMBA…MGUNDA KAFUNGA MACHO KISHA AKASEMA HILI KWA MATOLA…


Kocha mpya wa Simba, Juma Mgunda amesema anajua ana kibarua kigumu cha kuisaidia timu hiyo, lakini kupewa majukumu hayo haoni ni kitu cha ajabu.

Mgunda ambaye ametokea Coastal Union ya Tanga, amesema kocha kuhama timu moja kwenda nyingine siyo kitu cha sapraizi, bali kazi yao inahitaji utayari muda wote.

“Kazi ya wachezaji, makocha wanahitaji utayari wa kufanya kazi muda wote, ndicho kilichotokea kwangu, kikubwa ni Mungu anisaidie kuyafanya majukumu hayo kwa ushindi,” amesema.

Pia amesema ndani ya kikosi cha Simba yupo kocha msaidizi Selemani Matola ambaye alikuwa naye Stars, hivyo anaamini watashirikiana kuhakikisha wanayakabiri majukumu yaliyopo mbele yao.

“Matola namfahamu vizuri utendaji kazi wake, kwani nilikuwa naye Stars, pia ni mdogo wangu, ila kwa sasa akili zetu zinawaza kazi zaidi mengine yakae kando,” amesema.

Mgunda ndiye amekiongoza kikosi cha Simba kwenda Malawi, kucheza mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) dhidi ya Nyasa Big Bullets, mchezo huo utapigwa Jumamosi, saa 10: 00 jioni.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO JINSI MAYELE ALIVYOMKIMBIZA MZEE MPILI MJINI...ALIPIGA SANA PESA ..AKIMPINGA HERSI ATAKUWA KITUKO...