Home Habari za michezo BAADA YA KUPITIA MAGUMU….RONALDO AWEKA REKODI MPYA ULAYA…APIGA GOLI LA 700 MAN...

BAADA YA KUPITIA MAGUMU….RONALDO AWEKA REKODI MPYA ULAYA…APIGA GOLI LA 700 MAN UTD WAKIOSHA NYOTA ….


Nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo, amefuta ukame wa mabao ndani ya miaka 16 aliyokipiga baaa ya kufunga bao kwa mkwaju wa penalti dhidi ya Sheriff Tiraspol, kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Europa uliyochezwa jana Alhamisi.

Ronaldo amefunga bao hilo kwa mara ya kwanza kwenye mashindano hayo na kuweka historia maisha ya soka lake kwani hakuwahi kucheza michuano ya Europa tangu anaanza kucheza soka. Mkali huyo kutoka Ureno ana historia nzuri ya kushiriki michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya mara nyingi zaidi.

Ronaldo aliweka rekodi mbovu ya kutocheka na nyavu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006,  ikumbukwe aliwahi kucheza mechi 10 mfululizo bila bila kufumania nyavu kuanzia Machi hado Mei. Baada ya bao hilo Ronaldo amefikisha jumla ya mabao 700 kwa ngazi ya klabu.

Kocha wa Man United, Erik ten Hag amemtabiria Ronaldo atafunga sana msimu huu licha ya kuanza kwa kusuasua lakini amewaondoa shaka mashabiki wa timu.

“Tulitarajia haya kwasababu alikosa mechi za maandalizi ya msimu mpya, atafunga mabao mechi zinazofuta,  anajituma sana na anaendana na mpango yangu,  ameonyesha muunganiko mzuri, atakuwa fiti taratibu na atafunga sina shaka kabisa,” alisema Ten Hag.

Ronaldo alitishia kuondoka dirisha la usajili kiangazi mwezi uliyopita akatafute timu inayoshiriki Ligi Mabingwa Ulaya hata hivyo mpango wake ukagonga mwamba. Taarifa zimeripoti wachezaji wenzake walichangia kumshawishi Ronaldo abaki Old Trafford.

SOMA NA HII  JWANENG WAMEKUJA WAKATI MBAYA SANA ...TUTAWAPIGA KAMA NGOMA...- AHMED ALLY