Home Habari za michezo BAADA YA KUTOKA SARE NA AZAM JUZI…MABOSI YANGA WACHACHAMAA …ZAHERA ‘AMCHANA’ NABI...

BAADA YA KUTOKA SARE NA AZAM JUZI…MABOSI YANGA WACHACHAMAA …ZAHERA ‘AMCHANA’ NABI UWEZO WA LOMALISA…


YANGA imeangusha pointi mbili za kwanza katika Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya sare ya 2-2 na Azam FC, japo imeendelea kushikilia rekodi ya kutopoteza mechi 40, lakini mabosi wao kuna kitu wamekishtukia katika kikosi hicho.

Mabosi wa Yanga wameshtukia kitu kama ambacho mashabiki wao wamekiona kwamba kuna shida katika safu yao ya ulinzi hasa baada ya kubadilishwa kwa kitasa wao Yannick Bangala kutoka kiungo hadi kuwa beki wa kati.

Awali msimu uliopita Bangala alicheza sambamba na kiungo Khalid Aucho katika kiungo mkabaji na kuleta utulivu kwa mabeki wao wa kati.

Tangu Bangala aanze kutumika kama beki wa kati Yanga imeyumba kwani katika mechi tatu za ligi imetoka salama mara moja pekee dhidi ya Coastal Union huku mechi nyingine zote ikiruhusu mabao ikiwa tayari imefungwa matatu, ikiwa na maana kila mechi imeruhusu bao moja.

Hatua hiyo imewaamsha mabosi wa Yanga na kuanza kufikiria upya kusaka beki wa kati wa maana ambaye atakuja kuongeza ugumu katika eneo la ulinzi.

Inafahamika kuwa  mabosi wa juu wa Yanga wamelijadili hilo masaa machache baada ya mchezo wa Azam.

“Tutatafuta beki wa haraka wa kati wako ambao tukiona wamepungua ubora tutaangalia uamuzi wa kuchukua lakini ni kweli safu yetu ya ulinzi imepungua makali,” alisema bosi huyo wa juu wa Yanga.

Mbali na kusaka beki huyo wa kati mabosi hao wamejipanga kuhakikisha wanaongea na makocha wao kumuulizia beki Ibrahim Bacca ambaye alionyesha uwezo bora katika mechi za mwisho msimu uliopita.

“Tuna yule Bacca hatutajua kwa nini bado anakosa nafasi tutazungumza na makocha na kama tukiona kama kuna haja ya kuzungumza naye kumjenga kiushindani tutafanya hivyo.

MSIKIE ZAHERA

Kocha Mwinyi Zahera aliyewahi kuifundisha Yanga alisema ameangalia mechi hiyo lakini akakazia lazima kazi ya kusaka mabeki wawili ifanyike.

Zahera ambaye yuko kwao DR Congo alisema ukiachana na beki wa kati pia upande wa kushoto nako kuna changamoto kama watacheza na timu yenye winga bora Yanga itapata shida.

SOMA NA HII  HAYO MAPOKEZI YA MAYELE HUKO MISRI, SIO POA UNAAMBIWA KAMA MFALME

“Nimeangalia hiyo mechi ilikuwa bora kiushindani, nadhani tumepata kipimo sahihi cha kujua ubora wetu, ligi ya hapo ilitakiwa kuwe na mechi kama hizo kama 10 zinasaidia kujua ubora wa timu yako,” alisema Zahera.

“Kule kushoto pia Lomalisa (Joyce) naye bado eneo lake timu pinzani zinapita sana akiwa anacheza yeye, nafikiri makocha wameyaona hayo na kuyafanyia kazi.”

Mchambuzi Ally Mayay, alisema Yanga inahitaji marekebisho katika nafasi ya ulinzi kabla ya klabu hiyo kwenda katika michuano ya kimataifa, hasa kwenye raundi ya kwanza.

“Angalia bao la pili dhidi ya Azam mabeki walikuwa wamesimama hivyo ni lazima wawe na nidhamu ya kukaba katika mashindano ya kimataifa timu pinzani zinatumia makosa hata kama dogo kwa kiasi gani,” alisema Mayay.