Home Habari za michezo EHE…KUMBE ULE USHINDI WA SIMBA JUZI DHIDI YA TZ PRISONS KUNA MENGI...

EHE…KUMBE ULE USHINDI WA SIMBA JUZI DHIDI YA TZ PRISONS KUNA MENGI YALIFANYIKA..? MKUDE KAFUNGA HAYA A-Z…


JONAS Mkude, kiungo wa Simba amesema uwa haikuwa kazi rahisi kushinda mbele ya Tanzania Prisons kutokana na ugumu wa timu hiyo.

Mkude alipachika bao la ushindi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, dakika ya 85 kwa pasi ya Kibu Dennis.

“Kucheza na Tanzania Prisons kunahitaji kujipanga na timu ambayo itapata nafasi inaweza kushinda hivyo tulifanya maandalizi mazuri na tulipambana kusaka ushindi,” amesema.

Ni bao la kwanza la Mkude kwenye ligi msimu wa 2022/23 akiwa na uzi wa Simba.

Pia ni mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Juma Mgunda kushuhudia wakipata pointi tatu kwenye mchezo wa ligi.

SOMA NA HII  MASTAA SIMBA SC WALA KIAPO KUMALIZIA KAZI YA DAR...HISTORIA KURUDIWA..?